ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 15, 2014

SHAMBA LA MWANADIASPORA MZEE TEMBA LAUZWA HUKU YEYE AKIWA NA HAKI ZOTE ZA KULIMILIKI SHAMBA HILO

Diaspora tunachangamoto nyingi zinazo tukabili ukiachia mbali swala la uraia pacha ambalo sasa tumewekwa kama raia wa kigeni kwenye nchi yako ya kuzaliwa na kinachoangaliwa zaidi ni kitu gani umeifanyia nchi yako japo ughaibuni umekuja kutafuta sawa na Mtanzania yeyote aliyetoka mkoani na kuelekea Dar es Salaam kwa lengo lilelile analofanya mwanaDiaspora anapokuja ughaibuni.

Tukiachana na hiyo stori ya uraia pacha ninataka kukujuzeni kuhusu hii stori ya shamba ya mwanaDiaspora mwenzetu Mzee Temba mkazi wa New York ambaye kwa maisha ya kufanyakazi na kuweza kudunduliza na hatimae mwaka 1998 alienda Tanzania na kuweza kununua shamba kutoka kwa mzee mmoja anayeitwa Chea maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam na shamba kumkabidhi mdogo wake Gerald Temba kwa ajili ya uangalizi.

Totauti na matarajio yake shamba hilo limeingia kwenye mgogoro mwaka huu wa 2014 kutokana na kujaribu kuuzwa mara kwa mara na mhusika mkuu anaedaiwa ni mwekiti wa eneo hilo la Goba anayejulikana kwa jina la Bernard Magaga.

Gerald Temba mdogo wa mzee Tamba alimweka jamaa aliyejulikana kwa jina la Mathias kwa ajili ya kufanya shughuli zake za kilimo na huku akiliangalia shamba hilo lakini Mathias alienda kinyume na makubaliano hayo badala yake na kwa kushirikiana na mwenyekiti huyo wa Goba waliamua kuliuza shamba hilo.

Mathias alipoulizwa mara ya kwanza alikataa tuhuma za yeye kuhusika na uuzwaji wa shamba hilo lakini kutokana kufikiria sana mwisho ulifanyika mpango wa kumtumia mwanamke ambaye alienda kufanyanae mazungumuzo huku akimrekodi bila yeye Mathias kujua ndipo alipotoa siri zote ya jinsi alivyoshirikiana na mwenyekiti huyo wa Goba nakufanikiwa kuuza shamba hilo jasho la mwanaDiaspora.

Kwa sasa hizi aliyeuziwa shamba hilo ameishaanza kufanya ujenzi na Gerald Temba amefungua kesi ili haki iweze kuchukua mkondo wake.

Hapa chini ni mzungumuzo yaliyofanywa kati ya mwanadada huyo na Mathias japo kidogo yana maneno mengine ya kikubwa Vijimambo inaomba radhi kwa hilo.

No comments: