ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 29, 2014

SHEIKH ALI MZEE COMORIAN AZIKWA LEO KWENYE MAKABURI YA WANGAZIJA, JIJINI DAR LEO

Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto),Waziri Mkuu Mstaafu,Dkt. Salim Ahmed Salim (wa nne kulia),Sheik Mkuu wa Tanzania,Shaaban Simba (wa pili kushoto) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mussa Salum (wa tatu kulia) wakijumuika pamoja na Waombolezaji wengine kwenye ibada ya Mazishi ya Sheikh Ali Mzee Comorian,katika makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo.
Masheikh wakijadiliana jambo kabla ya Mazishi ya Sheikh Ali Mzee Comorian,katika makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo.
Taratibu ya kuandaa Kaburi la Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian zikiendelea katika makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo,huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha.
Umati wa Waombolezaji ukiwasili kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo,tayari kwa kuhifadhi mwili wa Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian akiefariki Dunia jana.
Sehemu ya Umati wa Waombelezaji ukiwa umebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian ukiwasili kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo.
Waombolezaji wakiendelea na shughuli ya Mazishi ya Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo.
Baada ya mazishi waumini wa Kiislam walifanya zikri kwenye Kaburi la Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo.
(PICHA: OTHMAN MICHUZI/EMMANUEL MASSAKA)

1 comment:

Anonymous said...

Inna lillah waina aillahim rajiun,sote ndo nyumba yetu ya milele ikifika siku zetu tutakwenda huko.

poleni sana wafiwa wote ndugu na jamaa na watoto wa mfiwa na wake na waislamu wote wa kingazija na wasio wa kingazija.

Inna lillahi waina illahim rajiun.

salaam kutoka New York, Mt.Vernon.