Advertisements

Tuesday, December 2, 2014

TAARIFA YA MSIBA

Familia ya Captain Narcis Mapunda wa Mikocheni B (TPDC) Dar es salaam, kwa masikitiko na huzuni wanatoa taaifa ya msiba wa mtoto wao mpendwa;
ELIAS NARCIS MAPUNDA
Kifo hichi ilichotokea siku ya Ijumaa tarehe 28 November 2014 hapa jijini Dar es salaam. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Baba mzazi Captain Narcis Mapunda, pale mikocheni, Nyumbu Street  (pandisha mtaa wa mikocheni Wariob tokea Mwai Kibaki Rd, baada ya Kanisa la Mt Martha ingia mtaa unaofuata kulia).
Maandalizi ya awali yanalekea kuwa na ratiba ifuatayo ya mazishi; mazishi yatafanyika kinondoni Makaburi ya Jumuiya ya Madola (ndani ya ukuta) siku ya alhamisi tarehe 4 December 2014 majira ya saa 10 jioni (1600 hrs). Awali ya hapo kutakuwepo  misa fupi, chakula pamoja na za heshima za mwisho nyumbani kwa Capt Mapunda, ikifuatiwa na misa maalum pale jirani kanisa la Mt Martha.  Ratiba ya shughuli zote inatarajiwa kuanza saa 4.30 asubuhi ya siku hiyo (1000hrs).
Habari za msiba huu ziwafikie wana-Mapunda popote pale walipo pamoja na nduguwote na marafiki.

Waweza kumpigia Mama Suzanne Mapunda kwa kujua taarifa zaidi - 0754 884104.

No comments: