ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 12, 2014

VODACOM YATANGAZWA MSHINDA WA TUZO ZA MWAJIRI BORA 2014‏

Waziri Mkuu Mizengo Pinda(wapili toka kulia)akimkabidhi kombe la Mwajiri bora 2014 Ofisa Mkuu wa Idara ya rasilimali watu wa Vodacom Tanzania Dr.Fredy Mwita(watatu toka kushoto) waliloshinda toka chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) baada ya kuyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo katika hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam.Kampuni hiyo ilishinda tuzo mbalimbali katika Nyanja tofauti,Wengine katika picha kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho Almasi Maige na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifurahia ushindi wa tuzo ya mwajiri bora 2014 iliyotolewa na chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) baada ya kuyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo katika hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam, kampuni hiyo ilishinda tuzo mbalimbali katika Nyanja tofauti kwa mwaka wa pili mfululizo.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akijadili jambo na wafanyakazi wenzake Simon Martin(kushoto)na Gloria Mtui(kulia)wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za mwajiri bora 2014 zinazotolewa na chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) ambapo kampuni hiyo iliyashinda makampuni mbalimbali yaliyoshindanishwa kuwania tuzo hizo, kampuni hiyo ilishinda tuzo mbalimbali katika Nyanja tofauti kwa mwaka wa pili mfululizo.Hafla hiyo ilifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kimeitangaza kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Limited kuwa Mwajiri Bora mwaka 2014. Mwaka jana vilevile Vodacom ilishinda tuzo hiyo.Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda alikuwa mgeni wa heshima katika hafla ya ATE ya kutoa tuzo kwa waajiri bora kwa mwaka huu ambayo ilifanyika jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Hii ni mara ya pili mfululizo tunatunukiwa tuzo hii na ushindi huu unathibitisha kazi kubwa tunayofanya kuhakikisha Vodacom inaongeza ajira zaidi na kuchangia kupunguza tatizo la ajira nchini”, alisema Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania Rene Meza.

Vodacom Tanzania pia iliongoza kwa ushindi katika makundi ya Utendaji na Uongozi Bora, Utekelezaji Bora wa Kanuni ya Uajiri na Raslimali Watu, Utendaji wa Kazi kwa Ubora na Viwango na kuwa na waajiriwa wanaoleta tija katika utendaji wao wa kazi.

Meza alisema Vodacom inajivunia kwa heshima ya tuzo ya ATE ambayo imeipata na hii inazidi kuthibitisha dhamira ya kampuni ya kuchangia kuleta mabadiliko katika jamii inakofanyia biashara hapa nchini na siku zote itakuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko na kutoa huduma bora.

“Tuzo hii imezidi kututia hamasa ya kuwekeza katika wafanyakazi wetu, shughuli zetu, jamii iliyotuzunguka na mtandao wetu kwa sababu kazi tunayoifanya inaleta mabadiliko makubwa ndani na nje ya kampuni. Hivi sasa huduma za mawasiliano tunazotoa zimewarahisishia wananchi maisha kiasi kwamba zimekuwa sehemu ya maisha yao.

Kwa mafanikio haya yote tunayojivunia nayo waajiriwa wetu wamekuwa ndio nguzo kubwa na ndio maana tunazidi kufanikiwa na kuimarika siku hadi siku, anasema Meza.

Mwezi uliopita Vodacom ilitangazwa kuwa mshindi wa pili kwa makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini ikiwa ni kinara wa kulipa kodi katika sekta ya mawasiliano katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments: