Washindi wa shindano la kucheza muziki, The Band wakionyesha mfano wa hundi ya shilingi milioni 1 ya Kenya.
Kundi la kucheza muziki lililokuwa likiwakilisha Tanzania, T-Africa likiwa katika pozi kusubiri matokeo.Katika fainali hizo zilizofanyika jana saa nne usiku moja kwa moja kupitia Runinga ya Citizen TV ya Kenya, kundi la The Band kutoka Kenya liliibuka kidedea ikiwa ni mara yao ya tatu kushiriki na kuambulia patupu kila mara ambapo jana usiku lilifanikiwa kujizolea kiasi cha milioni 1 za Kenya (sawa na shilingi mil. 18 za Kitanzania) wakati washindi wa pili wakiwa kundi la IDU la Uganda ambao walijizolea kiasi cha shilingi za Kikenya 300,000 (sawa na shilingi mil. 5,400,000 za Kitanzania) na ushindi wa tatu ulienda kwa kundi kutoka Tanzania la T-Africa waliojizolea kiasi cha shilingi 200,000 za Kenya (sawa na shilingi mil. 3,600,000 za Kitanzania).
Makundi mengine yaliokuwa yameshiriki ni pamoja na Wakali Sisi, Tatanisha, Al Pacino, DSI, Shakers, Limbo na mengine kibao yote kutoka Afrika Mashariki. GPL





1 comment:
vijana ndo taifa la kesho kuijenga nchi yetu na kuondoa ufisadi uliokithiri kila pembe ya nchi yetu leo wanashobokea kwa sana mambo yakukatika viono watoto wa kiume na anasa za jinga jinga sana.
hasara kweli.
Post a Comment