ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 28, 2015

AFCON: Ghana na Algeria zasonga mbele

Timu ya Taifa ya Ghana "Black Stars"

Ghana na Algeria zimesonga mbele hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kutoka kundi C.

Ghana imesonga mbele hatua hiyo baada ya kuibamiza Afrika Kusini Bafabana kwa jumla ya magoli mawili kwa moja.

Goli la kwanza la Ghana limefungwa na John Boye kabla ya lile lilolowavukisha Ghana kwenda hatua ya robo fainali lilil0tiwa wavuni na Andre Ayew katika dakika ya 83.

Goli pekee la Afrika Kusini limefungwa na Mandla Misango.

Nayo Algeria imesonga hatua hiyo ya robo fainali kutoka kundi hilo la C kama kundi la kifo baada ya kuibamiza Senegal kwa jumla ya magoli mawili kwa nunge.

Mchezaji wa Leicester City Riyadhi Mahrez alifunga goli la kwanza huku la pili likitiwa kimiani na mchezaji mwingine anayechezea England Tottenham Nabil Bantaleb.

Leo kutakuwa na mechi nyingine za mwisho kwa upande wa kundi D ambapo Cameroon watamenyana na Ivory Coast katika mechi wengi wanayoifananisha na fainali huku Guinea itakutana uso kwa uso na Mali

BBC

No comments: