Advertisements

Thursday, January 8, 2015

BAN KI MOON ASIKITISHWA NA ONGEZEKO LA MASHAMBULIZI DHIDI YA WALINZI WA AMANI NA WATOA MISAADA YA KIBINADAMU

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon pamoja na washiriki wa hafla ya kuwakumbuka walinzi wa amani wakisimama kwa dakika moja kuwaenzi walinzi wa amani na watoa misaada ya kibinadamu ambao ni wafanyakazi wa umoja wa mataifa waliopoteza maisha wakati wa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini Haiti mwaka 2010 na wale ambao wamepoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014.
Ban Ki Moon akizungumza wakati wa hafla hiyo ambayo iliibua hisia na majonzi makubwa miongoni wa washiriki wa hafla hiyo ya kuwaenzi walinzi wa amani na watoa misaada ya kibinadamu waliopoteza maisha wakati wakitekeleza wajibu wao wa kuwasaidia wananchi waliokuwa matatizoni. Miongoni mwa wahanga hao waliokumbukwa katika hafla hiyo ni Mashuja Watatu Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) waliopoteza maisha wakati wakitimiza wajibu wao katika Misheni ya Kulinda Amani ya MONUSCO katika Jamhuri ya Kidemokraria ya Kongo. Mashujaa hao ni Luteni Rajabu Mlima, Private Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian Msigila
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akitoa heshima zake mbele ya mshumaa mkubwa ambao uliandaliwa kama ishara ya kuwakumbuka na kuwaenzi Walinzi wa Amani na Watoa Misaada ya kibinadamu waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao katika kipindi cha tetemeko la aridhi lililotokea mwaka 2010 huko Haiti na wale waliopoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014. katika kipindi hicho Tanzania ilipoteza mashujaa wake watatu waliokuwa wakihudumu katika Misheni ya MONUSCO huko DRC

Na Mwandishi Maalum

Umoja wa Mataifa jana Alhamisi umewakumbuka walinzi wa Amani   na  wafanyakazi ya umoja wa mataifa waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yako katika kipindi cha Octoba 2013 na November 2014.
 Kumbukumbuka hiyo  imefanyika  katika siku  kama ya jana ( January 8) miaka mitano iliyopita  palitokea   tetemeko kubwa la ardhi huko Haiti na  kupoteza  maisha ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo  pamoja  na  uhalibifu  mkubwa wa  mali ilivuta hisia za waliohudhuria hata baadhi yao kutokwa na machozi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki  Moon akizungumza katika hafla hiyo amesema,  anasikitishwa sana na  ongezeko  la mashambulizi yanayofanywa  dhidi ya walinzi wa Amani pamoja na watoaji wa misaada ya kibinadamu ambao ni wafanyakazi wa  mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
Jumla ya  wahanga 102 walipoteza maisha nchi Haiti   wakati lilipotokea tetemeko hilo mwaka 2010,  huku wengine 100 walipoteza maisha kati ya Octoba 2013 na Novemba 2014. Wahanga hao  ni walinzi wa Amani na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa  kutoka mataifa mbalimbali duniani  na walikuwa wakihudumu katika Misheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa  na Mashirika yake.
Kati ya   waliokumbukwa jana wapo walinzi wa Amani watatu kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walipoteza maisha huko  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walikokuwa wakihudumu katika Misheni ya MONUSCO.
Mashujaa hao wa kitanzania   na ambao majina yao yalisomwa moja  baada ya jingine sambamba na  mashujaa wenzao wengine. Ni Luteni Rajabu  Mlima,  Private Mohamed John Mbizi na Private Vasco Adrian Msigila.
Ban Ki Moon amesema   walinzi  wa Amani na watoaji wa misaada ya kibinadamu wamekuwa wakipoteza maisha katika mazingira ambayo ukiacha yale yatokanayo ya majanga asili yakiwamo magonjwa ya milipuko na ajali, wengine wamepoteza maisha kwa mashambulizi yanayofanywa kwa makusudi. 
Na kwa sababu hiyo Katibu Mkuu anasema,  Umoja wa Mataifa unaendelea na jitihada zake za kuimarisha   ulinzi wao    ikiwa ni  pamoja na kuwajengea mazingira salama ya utendaji kazi  yakiwamo  mafunzo na vifaa 
Ameongeza kuwa  ushirikiano na michango kutoka nchi wanachama wa umoja wa mataifa ni  muhimu sana  hasa katika kipindi hiki ambapo siyo tu pamekuwapo na ongezeko kubwa la mahitaji ya walinzi wa Amani na watoaji wa misaada ya kibinadamu, lakini pia kutokana na ongezeko la  mashambulizi  dhidi yao na mazingira magumu ya kazi.

2 comments:

Anonymous said...

R.I.P mashujaa wetu na wengine wote walopoteza maisha yao.

Anonymous said...

Hasante Umoja wa Mataifa kuwaenzi maahujaa