Advertisements

Saturday, January 31, 2015

DIAMOND ALICHOKISEMA KUHUSU EX WA ZARI


Stori: Musa Mateja/Risasi
ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati aliamua kumtolea uvivu, aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’, King lawrenc kwa kumuita mpuuzi anayetafuta kiki kwa vile kila kukicha kazi yake ni kumfuatafuata kwa maneno ya kejeli na kumtusi.

X wa Zari, King lawrence akipozi.

Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, staa huyo alisema mara nyingi amejitahidi kumpuuza kwa kitendo chake cha kumkejeli katika mitandao ya kijamii, lakini kitu alichogundua ni kwamba mpenzi huyo wa zamani wa Zari anataka yeye amjibu ili aweze kulikuza jina lake, kitu ambacho ni cha kijinga.
Zarinah Hassani ‘Zari’.
“Nimejitahidi sana kukaa kimya kila anaponitusi huyu jamaa, lakini kumbuka mimi ni binadamu, najaribu kuliangalia jambo hili nagundua kwamba hana chochote cha msingi anachoongea zaidi ya matusi, anatafuta nimjibu kitu ili apate kiki aweze kutimiza ndoto zake,” alisema Diamond na kuongeza:
ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Zari.
“Nashukuru nimegundua hana mada ya kuzungumza katika mitandao zaidi ya mimi na Zari, ningemshauri aendelee na shughuli zake za kila siku, asihangaike na kitu asichokijua, kugombana na mimi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, mimi nawaza nifanyeje ili niweze kuitangaza nchi yangu, yeye anawaza afanyeje ili aweze kupandisha jina lake, siwezi kubishana na mpuuzi.”

Mwanaume huyo Mganda, kwa muda mwingi amekuwa akiweka picha zake, Zari na Diamond akisindikiza na maneno ya kejeli na dhihaka dhidi ya mkali huyo wa Bongo Fleva, katika kile kinachoonekana kuwa ni kushikwa na wivu.

1 comment:

Anonymous said...

bora umefanya laa maana kumpuza diamond but unamoyoo aiseee.jamaa anakutukana sana kabisa aaaah ningekuwa mimi angeshika adabu zake na kwa hasira ningejitahidi nimzalishe kabisa zari but najua hataki tena kuzaaa but ningembebeeza mpaka namzalisha tena ma twins na ashike adabu zake huyo kingi chambaz.

sijui zari alimpendea nini hata mvuto hata kidogo na kinaonekana kazee kazee hiviiii.

mzalishe wangu mzalishe zari atashika adabu zake huyu king.