ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 8, 2015

DIAMOND PLATNUMZ KUFANYA MAKAMUZI KATIKA UTOAJI TUZO ZA MWANASOKA BORA WA AFRIKA NCHINI NIGERIA LEO

Diamond Platnumz akifurahia jambo na mmoja wa wasanii wa Kundi la P Square, Peter Okoye wakati akijiandaa kwa ajili ya shoo yake ya leo nchini Nigeria.

Diamond akibadilishana mawazo na mwanamuziki Fally Ipupa jijini Lagos.


MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' leo atakinukisha katika sherehe za utoaji tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2014.

Zoezi hilo litafanyika leo Januari 8, 2015 jijini Lagos nchini Nigeria kuanzia majira ya saa 3 usiku.

Wakali wengine watakaokuwepo kutoa burudani leo ni pamoja na P Square, Flavour, Uhuru, Fally Ipupa na wengineo.-GPL

6 comments:

Anonymous said...

diamond vicheko vyote hivyo wakati kizungu chenyewe hukijui inakuwaje au mnigeria huyo anajua Kiswahili.msituzuge bwana diamond kizungu hajui hana kicheko hapo

Anonymous said...

diamond vicheko vyote hivyo wakati kizungu chenyewe hukijui inakuwaje au mnigeria huyo anajua Kiswahili.msituzuge bwana diamond kizungu hajui hana kicheko hapo

Anonymous said...

acheni wivu. sasa ndio amecheka umetamani kuwa wewe, we kalagha bagho

Anonymous said...

We kama kizungu unakijua mbona umeandika hicho kiswahili.acha kutukuza uzungu.kwa taarifa yako Huyo mkongo hata kusoma maelezo yaliyoandikwa kiswahiliii hujui Au ndo stress za.........

Anonymous said...

Diamond wa watu angekiogopa kingereza hangefika hapo leo.Kingereza kingereza wimbo usioisha,tuache kutafuta makosa jamani.Kingereza hatujazaliwa nacho na hakituzuii kusonga mbele na maisha.I'm proud of Diamond sababu amekubali kujaribu na si kuogopa.Diamond your good learn as you go buddy don't stop.Do your best don't worry.
Joanna

Anonymous said...

kizungu ndo kila kitu hata kama hujazaliwa nacho labda hujasoma secondary na chuo kikuu ndo maana unaona kizungu hakina deal ukisoma na kupita huko kote utajua kwa nini kizungu kina deal na aibu tena sana hata wakuu wetu wakija hapa kubongo kizungu kinawashinda what a shame.

msio soma ndo mtaona kizungu hakina maana waliosoma wanajua umaana wake wa lugha hiyo.

achene kumpotosha mwenzenu kama mnampenda kweli mwambiyeni ajifunze kizungu.

na hakuna anaye wifu na diamond kwa lipi mtu akukukosoa usiona kama anawivu na wewe au anakuchukia anataka kukurekebisha na ndo anayekupenda huyo.

acheni zenu hizo kama mnampenda kweli diamond mpeni ushauri mzuri ajifunze kizungu;kampata zarina amwambiye amfunze na kiganda pia.