ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 17, 2015

Gusa Gusa Min band ndani ya Usiku wa Old is Gold Safari Carnival Jumapili hii

NA ANDREW CHALE
BENDI ya taarab ya 'Gusa Gusa Min Band,' inatarajiwa kurindima tena Jumapili hii katika usiku wa Old is Gold Taarab , ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, uliopo Mikochezni B, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa waandaji wa usiku huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, kila Jumapili bendi hiyo ya Gusa Gusa imekuwa ikitoa burudani ya kipekee kwa nyimbo za taarab zikiwemo za zamani na zile za kisasa huku ikikusanya mashabiki lukuki.

Aidha, alisema muimbaji mwalikwa anatarajiwa kuwa Mohd Ilyas ‘Mfalme wa Old Is Gold’ kutoka Zanzibar ambapo atakuwa sambamba na Muimbaji Afua Suleiman .

"Kila jumapili kwa kiingilio cha sh 5,000 tu. Wapenzi wa muziki wa mwambao watafurahia bendi ya Gusa Gusa ndani ya Usiku wa Old is Gold ndani ya ukumbi wa Safari Carnival” alisema Asia Idarous.

Asia Idarous amewasihi wapenzi na wadau kujitokeza kwa wingi kushuhudia bendi hiyo pamoja na kukumbushana yale ya zamani na kubadilishana mawazo.

Mdau huyo Asia Idarous aliongeza kuwa, usiku huo uliodhaminiwa na Safari Carnival, Fabak fashions, Clouds fm, Gone Media, Maji Poa, Michuzi Media Group na wengineo, utakuwa wa aina yake kwa kila atakayefika ukumbini.

No comments: