Advertisements

Tuesday, January 20, 2015

HII HAPA INAMHUSU YULE KIKONGWE ALIYEVUNJA HISTORIA KWA KUJIANDALIA JENEZA, HIZI HAPA SABABU ZINAZOMFANYA AJIANDAE KWA KIFO

Mkazi wa Kijiji cha Lundusi, Kata ya Peramiho, wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, Bibi Scholastica Mhagama amejiandalia jeneza lake ambalo litatumika kumzikia siku atakayoaga dunia. 
Bibi Scholastica Mhagama(76) ambaye amejiandalia jeneza lake litakalotumika kumzikia.Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Scholastica alisema alilitengeneza jeneza hilo zaidi ya miaka mitano iliyopita baada ya kuona anaishi kwa dhiki na anatengwa na baadhi ya watu.
“Nilijitengenezea jeneza langu na fundi alipomaliza kazi, niliingia ndani kupima kama ninatosha, nikajilaza na kuona liko sawasawa,” alisema bibi huyo.
Bibi Scholastica Mhagama akiliangalia jeneza lake.Akifafanua zaidi bi mkubwa huyo alisema ameishi maisha ya dhiki na kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi, hali ambayo imemfanya amuombe Mungu amchukue ili azikwe kwenye jeneza alilojiandalia. “Kila siku naomba Mwenyezi Mungu anichukue haraka ili nikapumzike kutokana na mateso ninayoyapata, lakini hofu yangu ilikuwa je nikifa, nitazikwa kama binadamu wengine? Ndiyo maana nimeamua kujiandalia jeneza langu,” alisema bibi huyo mwenye ulemavu wa mguu uliotokana na kung’atwa na nyoka kisha kukatwa huku mwingine ukimsumbua kukunjuka.
Bibi Scholastica Mhagama akiwa ndani ya nyumba anayoishi.Alipoulizwa sababu ya kutengwa na jamii, bibi huyo alisema: “Nimetengwa na jamii na majirani wanashindwa kunisaidia wanadai eti mimi ni mchawi kwa sababu watoto wangu wote wanne walikufa wakiwa wadogo. Naumia sana kusingiziwa kitu ambacho sikijui.’’ Bibi huyo anayeishi katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi anasema kuwa, aliweza kutengeneza jeneza hilo baada ya kupewa shilingi 40,000 na mfadhili mmoja. “Tayari nilikuwa na mbao, hivyo kazi ilikuwa kumlipa fundi fedha na kumpa mbao ili anitengenezee jeneza,” alisema Scholastica. Bibi Scholastica akiwa nje ya nyumba yake siku alipoongea na mwandishi wetu.

5 comments:

Anonymous said...

Sasa unatoa mawazo gani ya kumsaidia au unapamba blog tu kwa shida zake?!!!. Wabongo bwana. Ah.

Anonymous said...

Huyu bibi anayo akili sana. Nina imani kwa upendo wa Mungu anemuomba kila siku atapata msaada mkubwa zaidi kuanzia sasa.

Anonymous said...

we mchangiaji wa kwanza mwenye blog kashachangia kuweka hii habari hapa. sasa ni jukumu lako mimi na wewe kusaidia kuwaelimisha watu wenye imani potofu kama hao anaokanaa nao karibu.

Anonymous said...

Huzuni but kwa nguvu za mungu she will get there...
Machozi yamenitoka natamani I could give her a hand but how. God bless this woman

Anonymous said...

Jamani ni uchungu mkubwa kutengwa na jamii sasa basi serikali yetu inatakiwa kuingilia kati tuna masocial worker wa serikali wapewe taarifa hizi kupitia wajumbe wa nyumba kumi. Hadi bibi huyu kuamua kujitengenezea sanduku la kumzika atakapokufa kweli amepata matatizo makubwa afanyiwe counseling na pia kwenye vijiji wananchi waelimishwe