Hitma ya Marehemu Jamila Simba Sakapala iliyofanyika Jumamosi Januari 17, 2014 Wheaton, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki. Marehemu Jamila alifariki ghafla siku ya Jumamosi Desemba 13, 2014 Tanzania na kuzikwa Jumatatu Desemba 15, 2014 watatu toka kushoto ni dada ya marehemu Zawadi Sakapala Ukondwa anayeishi Maryland nchini Marekani.
Wapili toka kulia ni kaka ya marehemu Simba Sakapala akiongea na mchungaji John Mbatta (mwenya miwani) siku ya Jumamosi Januari 17, 2015 siku iliyofanyika hitma ya Jamila Simba Sakapala aliyefariki ghafla Desemba 13, 2014 na kuzikwa Desemba 15, 2014 Tanzania.
Watanzania na marafiki zao wakijumuika pamoja na wafiwa kwenye hitma ya Jamila Simba Sakapala iliyofanyika Wheaton, Maryland siku ya Jumamosi Januari 17, 2015.
Watanzania wakijumuika pamoja na wafiwa kwenye kisomo cha Jamila Simba Sakapala kilichofanyika siku ya Jumamosi Januari 17, 2015 Wheaton, Maryland nchini Marekani.
Kisomo cha hitma ya Jamila Simba Sakapala ikiendelea Wheaton, Maryland nchini Marekani. Kwenye picha ni Eric (kushoto) na mume wa dada ya marehemu Faraja Rashid Ukondwa(mwenye kanzu)
Watanzania na marafiki zao wakiwa wamejumuika pamoja kwenye hitma ya marehemu Jamila Simba Sakapala kilichofanyika Wheaton, Maryland nchini Marekani. Wakwanza kulia ni shangazi wa marehemu Bi. Haiba Mfaume.
Wapili toka kulia ni mama yake mzazi Zawadi Sakala Ukondwa akiwa pamoja na Watanzania waliojumuika pamoja nao kwenye Hitma ya Jamila Simba Sakapala iliyofanyika Jumamosi Januari 17, 2015 Picha zote na Mubelwa Bandio
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
4 comments:
Tuendelee na mshikamano na upendo wetu bila kujali imani zetu! Inshallah mungu aendelee kutuongoza. Kisomo kilikuwa kizuri na mwenyezi mungu amrehemu dada yetu na ampe pepo njema. Amina
Inatia moyo sana kuona umoja wa watanzania unavyo vunja mipaka ya itikadi, dini na kadhalika. Ndugu zetu ni kweli tuendelee kushirikiana katika shida na furaha. Dada yetu amepumzika kwa amani kabisa. Kisomo kili kuwa kizuri na sisi ndugu tulifarijika sana.
waislamu mshikamane hivi hivi na kuishika dini yenu pia na kuisoma inafurahisha sana kuona mlivyojumuika pamoja. Allah amaleze maahali pema peponi dada yetu amina thuma amin
Mdau wa watu acha ubaguzi wa dini hatuna hy tanzania, kwani ina maana waliohudhuria wote ni waislam? Hebu kuwa makini na maneno yako unayoandika inaonyesha ni jinsi gn ulivyo mbaguzi wa dini Allahhapendi hivyo.
Post a Comment