Leo hii kwenye Live Chumba cha Habari tunaye mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Rashid Sultan ambaye amekuwa ndiyo habari ya mjini sasa hivi baada ya kujishindia kitita cha shilingi milioni 510 na kuahidi kurudisha nguvu zote kwa Waafrika ambao wamebadilisha maisha yake.
Katika mahojiano na safu hii ambayo huwa inarushwa kupitia Global TV Online kwenye Kipindi cha Mtu Kati, Idris alifunga zaidi;Mwandishi: Uliianzaje safari yako ya Big Brother?
Idris: Siku ya usahili nilifika mapema pale New Africa Hotel, namba yangu ya ushiriki ilikuwa 49 na washiriki tulikuwa wengi sana. Nikafanikiwa kumaliza awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu nikatakiwa kwenda Afrika Kusini. Ikafika siku ya kwenda nikaenda, nikafanya usahili tena nikarudi kusubiria majibu na baada ya wiki mbili-tatu hivi Mungu alibariki nikachaguliwa kwenda na mwisho wa siku nikashinda.
Mwandishi: Je, ni vigezo gani vilikufanya ukachaguliwa na kuwa mshiriki?
Idris: Ni kigezo kimoja tu ambacho mimi naweza nikasema kinajumuisha vigezo vyote ni kuwa wewe kama wewe, naamini ukichaguliwa kwenye usahili majaji wanataka muonekano wa aina fulani ambao utakufanya uwe mshiriki na ukifika kule usije ukaonesha kitu kingine tofauti, onesha kilekile ambacho ulikifanya pale kwa kuwa wewe tangu mwanzo na hicho ndicho kilichonifanya nikashinda.
Mwandishi: Kwa nini watu wakifika kule huwa na muonekano tofauti na maisha yao halisi?
Idris: Hivyo vitu vinatokea na huwa vinatokea wiki za mwanzo watu wanakuwa na muonekano tofauti kwa sababu kila mtu anafikiria anahitaji kuwa na muonekano wa aina fulani ili aweze kubadilika.
Mwandishi: Ulikuwa unalichukuliaje suala la kuoga mchanganyiko?
Idris: Muda wa kuoga ni mmoja ni namna ambavyo tulikuwa tunajipangilia wenyewe kuwa waanze wanaume au wanawake na haikuwa lazima kuingia pamoja na unachokifanya ndani ya nyumba ni juu yako wewe mwenyewe kama ulivyoamua.
Mwandishi: Una mipango ya kufanya kazi Hollywood?
Idris: Nina ndoto kubwa ya kufika huko, nilivyofika kwenye ile nyumba nilikuwa nina kipaji cha kucheza lakini pia naamini niko vizuri kwenye uigizaji hata kutoka kwa Fig, Big, washiriki wenzangu, mwalimu mwenyewe anashangaa kwa hiyo ninahitaji kuendeleza hicho kitu.
Mwandishi: Mlikuwa mnaishi vipi ndani ya nyumba, na je, kuna mafunzo yoyote ambayo mlipewa kabla?
Idris: Hakuna mafunzo, ukishafika kule kila mmoja anapewa sheria yenye listi ambazo zinajulikana labda hutakiwi kuharibu vifaa vya ndani ya nyumba na vurugu hazihitajiki, vyote mnapewa na kusoma ndani ya wiki moja na hivyo vitu ndivyo tunaenda kuvifanya kule.
Mwandishi: Vipi kuhusu uhusiano wako na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’?
Idris: Mimi ni mpiga picha na msanifu kurasa, Lulu alikuwa anakuja nampiga picha na ni rafiki ambaye tumejuana kwenye kazi tu, sitaki kujua amejiwekaje.
Kwa mahojiano kamili tembelea
No comments:
Post a Comment