Advertisements

Thursday, January 29, 2015

Jela kwa kufichua siri za kutengeza nuklia

Pedro Leonardo Mascheroni alipatikana na hatia ya kujaribu kuuza siiri za Marekani za kutengeza zana za nuklia

Mwanasayansi wa zamani katika mahabara ya kitaifa mjini Los Amos nchini Marekani amefungwa jela miaka mitano kwa kujaribu kuipatia nchi ya Venezuela siri za kutengeza bomu la nuklia.

Pedro Leonardo Mascheroni alikiri kosa mwaka 2013 la kutoa siri kwa jasusi wa FBI aliyejidai kuwa afisa mkuu kutoka Venezuela.

Pedro Mascheroni, mwenye umri wa miaka 79,anatoka nchini Argentina.Mkewe pia alifungwa jela mwaka mmoja.

Mascheroni alikuwa anachunguzwa kwa karibu mwaka mmoja kabla ya kuchukuliwa hatua.

Shirika la ujasusi la FBI, lilinasa komputa, barua , picha na vitabu kutoka nyumbani kwa mwanasayansi huyo.

Kulingana na stakabadhi za mahakamani, bwana Mascheroni aliambia afisaa huyo wa FBI kwamba angeweza kuisiadia Venezula kutengeza bomu la nuklia kwa kipindi cha miaka kumi.Marekani imekuwa katika mstari wa mbele kupiga vita nchi zenye miradi ya kutengeza nuklia

Alisema nchi hio ingeweza kutengeza mtambo wa kisiri wa nuklia chini ya ardhi kuisiaidia kurutubisha madini ya Plutonium.

Aliongeza kwamba pia angeisaidia Venezuela kuzalisha kawi ya nuklia.

Bwana Mascheroni alifanya kazi kwa karibu miaka kumi katika kitengo cha kutengeza zana za nuklia katika mahabara ya kitaifa ya Marekani ambako bomu la kwanza la Atomiki lilitengezwa.

Mkewe alikuwa mwandishi wa maswala ya teknolojia katika mahabara hio.

Aliachishwa kazi mwaka 1988

Katika mahojiano na shirika la habari la AP, alisema alifanya mawasiliano na nchi nyingine baada ya wazo lake la kutengeza kawi safi ya nuklia kukataliwa na maafisa wa baraza la Congress.

Mascheroni alisema alifanya mazungumzo na Venezuela, baada ya Marekani kukata wazo lake la kuzalisha kawi safi ya nuklia.

Serikali ya Marekani,imesema kuwa haiamini kuwa Venezuela ilikuwa inajaribu kuiba siri zake za kutengeza zana za nuklia. BBC

No comments: