ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 2, 2015

JUMUIYA YA DMV YAUNGA MKONO MRADI WA MALARIA WA JENGA

Bwn. Nassoro Basalama Mkurugenzi wa JENGA Foundation akiwa na Mkewe walipohudhuria sherehe ya kuukaribisha mwaka 2015 DMV

Foundation ya JENGA yapokelewa na Jumuiya ya Washington, DC kwa mwamko mzuri wa lengo la kujishirikisha kusaidia nyumbani Tanzania katika masuala ya malaria. Mradi ambao ulielezewa na Mkurugenzi wa JENGA Bwn. Nassoro Bassalama kwa kina. Pia Mgen rasmi Balozi wa African Union Bi Amina S. Ali, alihamasishwa na JENGA juu ya mradi wa malaria na kuwasihi watanzania wajishirikishe kwa juhudi. Mhe. Kadari Singo, Mbunge wa Diaspora, naye alielezea jinsi gani malaria inavyomgusa binafsi.

Mkurugenzi wa JENGA aliwashukuru sana wana DMV na Media kwa kushirikiana na JENGA kwa kuhamasisha watanzania waliopo nje kujishirikisha kusaidia kwa pamoja kupunguza na hatimae kutokomeza ugonjwa wa malaria ambao umekua tishio kwa nchi yetu.

Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly alimpongeza Mkurugenzi wa JENGA Foundation Bwn. Nassoro Basalama na kumshukuru kwa kuja kwake na kujumuika na Watanzania wa DMV na kuwapa elimu kuhusiana na ugonjwa huo hatari wa Malaria na unavyoweza kupoteza uhai wa binadamu kwa haraka.

Mkurugenzi wa JENGA Bwn. Nassoro Basalama pia alionyesha kifaa cha kupimia ugonjwa huo wa malaria ambacho unaweza kukitumia nyumbani kwa kujipima mwenyewe bila daktari na kikakuwezesha kutambua kama unamalaria.

Jumuiya ya DMV ilikabidhi $200 kwa ajili ya kusaidia mradi huo.

2 comments:

Anonymous said...

Maendeleo na mabadiliko ya Tanzania yataletwa ns watanzania wenyewe

Anonymous said...

huyu baasalama he is a cute man.mmmh nammezea mate