Advertisements

Saturday, January 31, 2015

KITENDO HIKI CHA ZUA MJADALA HUKO TANZANIA JITIRIRISHE HAPA CHINI NA WEWE UNALA KUSEMA

Kwa wanamichezo ni kama kumpa moyo mchezaji mwenzie au kama pongezi.
Hapa ni rais Bush akimpongeza mchezaji wa timu ya taifa ya volleyball ya Marekani.
Hapa ni kocha wa timu ya taifa ya Cameroon
Beki wa Mbeya City Juma Nyosso.
Na Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya Gazeti la Championi kutoa picha ya beki wa Mbeya City, Juma Nyosso akionekana kumfanyia ndivyo sivyo straika wa Simba, Elias Maguri, makubwa yameibuka.


Uongozi wa Simba na Maguri wote kwa pamoja wametoa kauli juu ya tukio hilo na kulikemea kwa nguvu huku wakilishukuru gazeti hili kwa kutoa picha hizo kwa kuwa Watanzania na jamii nzima imejua ‘uchafu’ ambao unafanyika kwenye Ligi Kuu Bara.


Evans Aveva ambaye ni rais wa Simba, amesema tukio hilo lililotokea wakati wa mechi baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, ni la kidhalilishaji na kudai matukio kama hayo yanapingwa kwa nguvu zote na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).


“Sijui sana kuhusu maadili ya uandishi wa habari lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatakiwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya wachezaji kama hao.“Kimsingi suala hili la kuchapishwa picha za tukio alilofanyiwa Maguri katika Gazeti la Championi siwezi kulizungumzia kitaaluma.


“Lakini tunakikemea vikali kitendo hicho, kwani tumesikitishwa sana. Hii ni changamoto kwa TFF na klabu kuhakikisha tunakwenda sambamba na teknolojia, tusisubiri mpaka ripoti za waamuzi ndipo tufanye maamuzi.


“Mfano ni suala la Suarez alipomng’ata mchezaji wa Italia, Fifa ilimfungia baada ya kutumia teknolojia na haikutumia ripoti ya waamuzi pekee. Matukio mabaya yamejitokeza kwa (Amissi) Tambwe, (Emmanuel) Okwi na Maguri, pia huko daraja la kwanza ndiyo usiseme.


“Ninavishukuru vyombo vya habari kwa kuweza kuibua mambo hayo ili yaweze kuchukuliwa hatua na kukomeshwa kabisa,” alisema Aveva. Akizungumzia tukio hilo, Maguri alikuwa na haya ya kusema: “Kwanza nikwambie tu ile ishu imenidhalilisha sana kwa watu wengi maana imekuwa ‘topic’ kubwa katika mitandao ya kijamii. Kwa hiyo mimi binafsi na familia tunalichukulia kama tukio baya sana kwangu kwani limetudhalilisha.


“Siwezi kuliacha hivihivi, lazima nilichukulie hatua lakini kwa vile TFF na wahusika wengine wameliona, ninasubiri kwanza kuona hatua gani watachukua, kama sitaridhika nazo ndipo nitakapojua nini cha kufanya.“Nashukuru mpigapicha wenu kwa kuwa alifuatilia na kuliona tukio vizuri japokuwa ni la aibu.” 

Kitendo cha Juma Nyosso ni cha kipuuzi na sio cha kiungwana.

1 comment:

Anonymous said...

kila kitu ruksa ruksa cha ajabu kipi si tunaiga mambo ya mamtoni majuu wa wenye mambo na technologia.
ichii watu wanakwapua pesa mchana kweupe,wauza sembe wanajulikana,

mapolisi wanawapiga wapinzani wamepewa ruksa NA WAPIGWEE,mwandishi wa habari aliuliwa,wachina njaaa njaaa arosto ndo wawekezaji wanachoma mahindi kariakoo wamekuwa chinga boys,

wakina dada hawajistiri wanavaa wanavyotaka ukienda kwenye club ndo utashangaa ngono nje nje.

ngoma za vigodoro vinapamba moto wakina mama wanajisebejua raha iliyoje,ruksa ruksa.

washenge, wasagaji ruksa wako kibao so chaajabu kipi.

wache wabahashianane kushikana makali; ndoa za jinsi mmoja hizo waache waendele tuu hakuna noma,hakuna vibaya hakuna cha ajabu wala cha kushtusha roho.mammbo poooooooooooooaaa mambo tambarare

ruksa ruksa mpaka hapo mungu atakapo tuletea mafuriko na mabalaa ya vimbunga na kufaa kwa sana ndo tutakuja kumjua mungu ndo nani na adhabu yake ikoje.

ruksa ruksa hakuna noma na wazidishe kwa sana kubahashiyana wenyewe kwa wenyewe tujue kidume cha mbegu nani .