ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 29, 2015

"TAAANZANIA TANZANIAAAAAA NAKUPENDA KWA MOYO WOTEEEEE", WIMBO HUU KWA SASA HAUNA MAANA TENA KUTOKANA NA UKATILI WA POLISI.

Video ya Maandamano ya CUF Temeke na Mhe. Ibrahim Lipumba alivyokamatwaVideo kwa hisani ya VOA


Mtafaruku tulioshuhudia jana bungeni wakati wabunge wa vyama vya upinzani waliposimamisha shughuli za Bunge na kusababisha kuahirishwa ni ushahidi tosha kwamba sasa vyama hivyo vimefika kikomo cha kuvumilia vitendo vya Jeshi la Polisi nchini dhidi ya vyama hivyo na wafuasi wake. Wabunge hao walisimama na kupaza sauti wakipinga vitendo vilivyofanywa na askari wa jeshi hilo jijini Dar es Salaam juzi vya kuwapiga, kuwadhalilisha na kuwakamata wafuasi na viongozi wa CUF, akiwamo mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba na kuwafikisha mahakamani kwa madai ya kufanya maandamano bila kibali cha polisi. Wabunge hao walimtaka Spika Anne Makinda kuitaka Serikali itoe tamko bungeni kuhusu unyama huo wa polisi dhidi ya viongozi hao. Maelezo ya Spika kwamba Serikali ingetoa tamko leo, yalikuwa kama yameongeza petroli kwenye moto, kwani wabunge hao waliendelea kupaza sauti kwa namna ambayo shughuli za Bunge zisingeweza kuendelea. Hoja yao ya msingi ilikuwa kwamba, katika kuwatia nguvuni viongozi hao, polisi walivuka mipaka kwa kuwadhalilisha, kuwapiga mabomu na virungu wakati ingetosha kuwaelekeza
kwenda wenyewe katika kituo cha polisi ili kuwahoji. Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia aliliambia Bunge kwamba polisi walipaswa kutambua nafasi ya Profesa Lipumba kama mwenyekiti wa chama chenye usajili, hivyo polisi walipaswa kumpa heshima stahiki badala ya kumdhalilisha. Siyo nia yetu kuhoji au kuunga mkono hatua hiyo ya wabunge hao, isipokuwa kusema kwamba nchi yetu bado ina safari ndefu kuelekea kwenye demokrasia ya kweli na utawala bora. Jambo lililo wazi ni kwamba hatua ya wabunge hao ni ya kukata tamaa kutokana na Jeshi la Polisi kuendelea kukandamiza vyama vya upinzani. Tunasema hivyo kwa kuwa jeshi hilo limekuwa likikiuka Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, ambayo inatoa uhuru kwa vyama vya siasa kufanya shughuli zake za kisiasa. Kwa mfano, haki ya kuandamana iko kisheria, hivyo polisi wanapozuia maandamano kwa kutoa sababu dhaifu wanavunja haki hiyo. Katika tukio la juzi, polisi walisema walikuwa wakitekeleza amri kutoka ‘juu’, CUF ilikuwa imeandaa maandamano ya kumbukumbu ya vifo vya wanachama wake 22 waliouawa na polisi kisiwani Pemba mwaka 2001 wakipinga matokeo ya uchaguzi. Polisi walizuia maandamano hayo kwa madai kwamba yangesababisha vurugu. Hawakusema kwa nini nguvu nyingi na silaha zilizotumika kuzima maandamano hayo, zisingetumika kutoa ulinzi kwa waandamanaji hao, kwani kuzima maandamano hakuwezi kufuta historia kwamba polisi waliua wafuasi hao wa CUF waliokuwa wakihoji uhalali wa matokeo ya uchaguzi huo. Miaka 22 tangu kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi nchini, jeshi hilo lililoundwa chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Jeshi la Polisi, Sura ya 322 sasa linaonekana kuacha misingi yake na kuchukua sura ya kisiasa. Limekataa kutambua kwamba sheria ya vyama vya siasa haitoi mamlaka kwa jeshi hilo kuratibu shughuli za vyama hivyo. Sheria inasema ili shughuli hizo zifanyike kwa amani na utulivu, jeshi hilo litapewa taarifa rasmi ndani ya saa 48 kabla ya kufanyika kwa shughuli hizo ili litoe ulinzi. Ni lini vitendo hivi vya polisi vitakoma? Wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu, kuna haja ya mihimili ya nchi kuliangalia suala hilo kwa makini na kuweka misingi ambayo italifanya Jeshi la Polisi lisitumike kisiasa katika utekelezaji wa majukumu yake. MWANANCHI

10 comments:

Anonymous said...

nimepata uchungu sana, kuona hiyo video du.! police brutality, I think we need to change the tone here. heshima haitakuwepo bila damu kumwagika, sacrifice needed for future generation.

Anonymous said...

This is indeed police brutality against humanity. Police should be there to protect people for peaceful demos. I am completely devastated by their actions on their fellow citizens beating people as if they are beating animals - you would not even be so rude to animals!! Your days (police) are numbered. Did you see what happened with the brutality in Libya or Egypt - the Arab Springs? Do you want this to come down to you - cruelty against fellow humans? This scenario shows how stupid you all are...

Anonymous said...

Very sad and shame on you leaders of this country!! Police acted v

Anonymous said...

Police acted very stupidly with unnecessary use of force. Poor citizens you have no right!! Ila hii inamwisho msifikiri kunakomwaga damu hawakuanza hivi

Anonymous said...

KWa hakika nimesikitishwa sana na matukio niliyoyaona katika video hii juu ya udhalilifu unaendeshwa na polisi,ambao ni chombo ambacho kinatakiwa kuwa mfano bora.

Huu ni uadui ambao unapandikizwa na polisi wetu, hauna nafasi na wala hautakiwi kuruhusiwa kwa taifa hili, kwani tabia hii inatudhaliisha sote.

Tanzania tumekuwa tukisifika kwa Amani na utulivu. Maana yake nikuheshimu watu na uhuru wa kujieleza na kuchagua.

Mimi ni mwana CCM, napinga kapisa kuwa huu sio muongozo wa chama chetu na wala pilisi hawajafanya, uhuni huu kwa niaba yetu.

Ni matumaini yangu chama change kitatoa tamko la kupinga udhalilishaji huu, ambao hauna tija wala sifa yoyote kwa nchi yetu.

Polisi napenda mfahamu, hamutuwakilishi katika hatua hizi, za uvunjaji wa haki za binaadamu na Zaidi wa demokrasia ambayo chama change cha CCM, kimekuwa mstari wa mbele kuijenga.

Napenda mfahamu kuwa hamuifurahishi CCM, kama wasivyokuwa hawaifurahishi CCM, wale ambao, wamekuwa wakihusika na rushwa.

CCM itaendelea kusimamia haki na kulinda aman, kwa kuheshimu watu hiyari ya mvuto wa kisiasa.

Naomba muwache na muombe radhi, kwa wananchi juu ya kutuchafulia jina letu. kwani moja katika matukio yanayokumbukwa ni mauwaji yaliyoshirikishwa polisi.

Mnapelekea chama chetu kinaingia doa kwa mambo mnayoyafana,na kuwapa fursa wapinzani kuyaunganisha maamuzi yenu na jina la CCM.

Anonymous said...

Jamani, Serikali ya Tanzania ipo wapi?, amiri jeshi mkuu kama huko uliko umeona haya na ukakaa kimya, basi Dunia itakushangaa na utakuwa hujawafanyia Wananchi wako Yale wanayoyategemea kutoka kwako.

Anonymous said...

This is so rued, Hakika Mungu hatowaacha mfaidike. You were supposed to ensure that every one there is safe rather than biting a human being like u what to kill an elephant.

Shame on you the leaders of this country and shame upon you wote mliousika kupiga watu.

Mind you no one will choose CCM in 2015 for God sake. We are done with this chama.

Mungu awaponye wote walioumia katika hili

Anicetus said...

Panda Gari-Panda gari- Panda Gari... Maneno ya Professor Limpumba: Watoto ammbao hawakuenda shule.. ndio hatari ya democracia

Anonymous said...

voice of America na vijimambo team ahsanteni sana kwa kutuwekea clip video hii.nilidhani wakina dj lucas ccm damu hawatutuwekea hii clip. ahsanteni kwakweli jamani mbarikiwe daima.

na point of correction nimeangalia zaidi ya mara mbili professor lipumba hajasema maneno hayo panda gari panda gari,maneno hayo ya mapolisi na wao ndo walio mwambia professor mzima unakuwa na hawa watoto wasioenda shule.

kwa hivyo msimlishe maneno professor lipumba bure.

na nauliza kuenda shule na kupata madegree na ma phd ndo mjanja msataarabu au ndo una akili sana.

na asiye soma hana busara hana akili?

bill gates vipi na mnamubudu,na wengi wengi tuu.

acheni kasumba ya kwenda shule walioenda shule na kupata ma phd ndo mafisadi wakubwa na hawana hata fikra hata ya kutengeneza tooth picks zinatoka Pakistan na vibiriti.usomi wao umepo wapi.

acheni zenu bwana.

Anonymous said...

na wapigwe tu bwana, si pinda alishasema hivyo.

hii yote hofu ya mafisadi maccm kuona wanashindwa na wapinzani na njia mmoja wapo ya kuwadhibiti.na polisi wanafanya jambo baya sana kutokuheshimu vyama vingi ambavyo kwenye katiba vimeandikwa.

mimi nimeshawapa notice wapangaji wangu wawili mapolis walio katika nyumba yangu waenda kwenye serikai yao wawapi nyumba zakukaa.

wanatutesa sisi bure basi waenda huko kwa ma ccm wenzao wanaowatuma kama misukule na kuwazarau.