ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 19, 2015

MBUNGE JAMES MBATIA AWASHUKURU WANANCHI JIMBO LA VUNJO KUKIUNGA MKONO CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

MBUNGE WA CHADEMA ARUMERU MASHARIKI JOSHUA NASSARI ASHIRIKI
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari akiwasili katika mkutano huo.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ,Ndolakindo Kessy akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ghalani ,mji mdogo wa Himo ,mkutano uliokuwa na lengo la kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Vunjo kukipa chama hicho viti vingi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji.
Mh Nassari na Mh Mbatia wakitoa salamu kwa mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo .
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza na wananchi katika jimbo la Vunjo,wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi kwa lengo la kuwashukuru kwa kuchagua wenyeviti wengi waliotokana na chama cha NCCR-Mageuzi,mkutano uliohutubiwa pia na Mbunge wa kuteuliwa na rais,James Mbatia.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ghalani katika mji mdogo wa Himo jimbo a Vunjo alipokuwa akiwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kukipa ushindi chama chake katika uchaguzi wa serikali za Mitaa ulimalizika hivi karibuni.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.






Mmoja wa wakazi katika jimbo la Vunjo ,Elizabeth Mrema akimkabidhi Mbunge wa kuteuliwa na rais ,Mh James Mbatia zawadi ya shati la Kitenge kwa niaba ya wakazi wa jimbo la Vunjo ,kuipeleka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu ,Joseph Waryoba.
Mmoja wa wakazi katika jimbo la Vunjo ,Elizabeth Mrema akikabidhi zawadi ya Suti kwa niaba ya wakazi wa Jimbo la Vunjo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuingia Bungeni kupitia uwakilishi wa Jimbo la Vunjo.
Mbunge Nassari akiwa na viongozi wa chama cha NCCR-Mageuzi wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi ,James Mbatia akitafakari jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ghalani ,mji mdogo wa Himo ,mkutano uliokuwa na lengo la kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Vunjo kukipa chama hicho viti vingi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji.
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,(Chadema) jimbo la Vunjo wakiteta jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ghalani ,mji mdogo wa Himo ,mkutano uliokuwa na lengo la kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Vunjo kukipa chama hicho viti vingi katika uchaguzi wa serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji.
Baaadhi ya viongozi waliochaguliwa wakati wa uchaguzi wa serikali za Mitaa,vijiji na Vitongoji uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Mamia ya wananchama na mashabiki wa chama cha NCCR-Mageuzi wakimsikiliza ,Mh Mbatia(hayupo pichani).Picha Na Dixon Busagaga wa Globu 


ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: