Advertisements

Thursday, January 29, 2015

MGANGA WA DIAMOND JELA MIAKA 7

Ustadh Yahya akiwa chini ya ulinzi.
Stori: Richard Bukos/Amani
Yule mganga aliyejitapa kumtengenezea nyota ya mvuto staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ustadh Yahya amehukumiwa kifungo cha miaka saba (7) jela baada ya kukutwa na hatia katika kisa cha kuchanganya akihusishwa na wizi wa gari.
TUJIUNGE MAHAKAMA YA WILAYA YA ILALA
Habari za uhakika zilieleza kwamba aliyehitimisha kesi hiyo ni Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar, Hassan Kisailo mapema Jumatatu wiki hii wakati jua la asubuhi likiwaka.
HAKIMU ASHUSHA MIWANI
Huku kijasho chembamba kikimtiririka huku akishusha miwani kidogo kuona wahudhuriaji wa kesi hiyo, Hakimu Kisailo alitoa hukumu hiyo kwa maelezo kwamba, mnamo Januari 20, mwaka jana, maeneo ya Kariakoo jijini Dar, Yahya alidaiwa kuiba gari aina ya Toyota RAV4 lenye namba za usajili T 139 BSJ likiwa na thamani ya Sh. milioni 12, mali ya Edrick Elieza.
Wakati Hakimu Kisailo akisoma hukumu hiyo, mshtakiwa na wadhamini wake hawakuwepo mahakamani hapo hivyo alisema mara tu baada ya hukumu wahusika hao watakamatwa ili wakatumikie adhabu inayowakabili.
MAPITIO MTIRIRIKO WA KESI
Huku akiangalia kulia na kushoto, Hakimu Kisailo alisema kuwa, baada ya kuupitia mtiririko wa kesi hiyo, alibaini kwamba ni kweli mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo hivyo alimhukumu kwenda jela miaka 7.
...Ustadh Yahya akilaumu 
Jambo.

Kama ilivyo desturi ya Magazeti ya Global kutaka kujua vitu kwa undani, mwanahabari wetu alizungumza hakimu huyo kuhusiana na hukumu hiyo ambapo alishusha tena miwani kidogo kisha kumwangalia kwa juu na kusema:
“Ni kweli huyo mnayemuita sijui Mganga wa Diamond nimemhukumu kwenda jela miaka 7, ingawa hakuwepo hapa mahakamani.
“Nasikia alitoroka tangu alipowekewa dhamana lakini kifungo hicho kitaanza muda wowote atakapokamatwa.”

WADHAMINI NAO WANALO
Hakimu Kisailo alisema kwamba, Ustadh Yahya aliwekewa dhamana na watu wawili, Moses Msangi na Seme Kisusandi ambao wanatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja au kwenda jela miezi sita wakati sangoma huyo akisakwa.

Hakimu Kisailo alisema licha ya jamaa huyo kuingia mitini, wadhamini wake nao hawakuwepo mahakamani hapo na kusema kuwa mkono wa sheria ni mrefu utawafikia popote pale walipo.

MANENO KUNTU
Mmoja wa mashuhuda wa kike aliyekuwa kwenye chumba cha hakimu huyo alisikika akisema: “Huyo mganga wa Diamond hana lolote, iweje ashindwe kuzima kesi yake na kufikia hatua ya kuhukumiwa kifungo hicho wakati huwa anajidai ni mkali kwenye mambo ya kuwatengenezea watu nyota?
“Unaweza kukuta huko mitaani anajifanya kuwaambia wateja wake ana uwezo wa kuzima ‘makesi’ makubwa-makubwa kumbe hata kesi yake mwenyewe inamshinda.”
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
DIAMOND ATUPIWA LAWAMA
Shuhuda huyo alikwenda mbele zaidi na kumtupia lawama Diamond kwamba alishindwaje kumsaidia mtu aliyempaisha hadi sasa hivi anawiki kimataifa?
DIAMOND ANASEMAJE
Amani lilimsaka Diamond ili kumfikishia ‘ubuyu’ kuwa mganga wake amehukumiwa miaka sasa jela lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata alipofuatwa nyumbani kwake, Sinza-Mori, Dar, hakuwepo.
TUMEFIKAJE HAPA?
Ustadh huyo alidaiwa kukamatwa na gari hilo alilodai kufika mikononi mwake kutoka kwa mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Mwanahamis. Ustadh alikamatwa akikatiza nalo Tabora mjini ndipo akawekwa nyuma ya nondo za mahabusu kabla ya kusafirishwa jijini Dar kwa hatua zaidi za kisheria ambazo zimemhukumu kifungo hicho.
Source:GPL

1 comment:

Anonymous said...

we shuhuda una wazim,km mtu alijihusisha na wizi iweje umlaumu Diamond,kwani alimyuma akaibe ata ampe msaada,kila mtu ataubeba mzgo wake,km Diamodn aipata huduma basi hakika alilimpa na mkataba uaisha,nyamaza km hauna la kusema usitafute kiki kwa kesi zisokuhusu.