ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 28, 2015

Mkutano Mkuu wa CHAUKIDU na Tamasha la ukuzaji Kiswahili kufanyika Washington DC

Aprili 23 mwaka huu, Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (chaukidu) kinategemea kufanya mkutano mkuu wake, pamoja na tamasha la ukuzaji wa lugha ya Kiswahili.
Hayo yatafanyika hapa Washington DC.
Septemba mwaka jana nilipata fursa ya kuhudhuria mkutano wa awali uliojadili mikakati ya mkutano na tamasha lijalo.
Baada ya hapo nilipata fursa kuzungumza na viongozi wa CHAUKIDU
Dr Leornard Muaka. Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chaudiku. Na ni mwalimu wa lugha katika Chuo Kikuu cha Wiston Salem jimbo la North Carolina
Dr Dainess Maganda. Yeye ni Mwana-bodi wa CHAUDIKU. Na ni mwalimu wa lugha, mtaalam wa ufundishaji wa utamaduni wa kiafrika katika chuo kikuu cha Georgia jimbo la Georgia
Karibu usikilize

No comments: