Japhet Kembo (Chadema) akila kiapo cha kuwa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Migombani kata ya Segerea wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam mbele ya wakili wa kujitegemea Idd Msawanga (mwenye suti nyeusi) leo Jumatatu Januari 19, 2015 nje ya ofisi hizo, jijini Dar es Salaam, tukio hilo ni la aina yake kwani kiutaratibu, mshindi huapishwa katika hafla inayoandaliwa na halmashauri ya wilaya husika. Hata hivyo, kumekuwepo na mizengwe ya kuapishwa kwa Japhet, ambapo viongozi wenzake kutoka kata hiyo tayari walikwisha apishwa wiki iliyopita katika hafla iliyoandaliwa na halmashauri ya wilaya ya Ilala na kufanyika kwenye ukumbi wa Anatouglu, Mnazi Mmoja jijini.
Japhet, akibebwa na wafuasi wake
Japhet, akipongezwa na Samwel Binagi, (Kushoto), mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa mtaa wa Migombani kupitia CCM, aliyeshindwa kwenye hatua ya kura za maoni za chama chake
Japhet, akishangiliwa baada ya pongezi kutoka kwa "wapinzani" wa jadi wa chama hicho Picha kwa hisani ya K-VIS Blog



No comments:
Post a Comment