Bwana George Mcheche Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya.
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Picha na IKULU
2 comments:
Kaka Luka..post hizi msg zingine unabania sana..viongozi wanasoma..mheshimiwa raisi kwa nini unatufanya watanzania wajinga ? Hivi kweli mama Tibaijuka peke yake ndio mwizi wankufungia mwaka? Kwa nini wengine wamebaki? Na kwa huyo mama haendi mahakamani wala kurudisha pesa basi ..yaishe..? Mi nafukiri ni hivi na wewe mheshimiwa raisi upo kwenye hii ESCROW ..au una beba marafiki..wizi acheni jamani..
Kubebana tuu watu washaaanza kusahau..short memory za kibongo mbaya sana..kila mtu kanyamaza anachagua mwanasheria mpya..? Halafu iweje
Post a Comment