Wakati kikosi cha Simba leo kikishuka kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kuumana na Ndanda FC ya mkoani humo, Uongozi wa klabu hiyo umempiga ‘stop’ kocha wake, Goran Kopunovic kuzungumzia ligi kuu mpaka baada ya michezo mitatu.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya klabu hiyo, Said Tully, alisema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa kuwa kocha huyo bado ni mgeni na ligi kuu.
Tully alisema kwa sasa kocha huyo hawezi kuzungumzia ligi kuu kwa kuwa aliwasili nchini wakati ligi hiyo imesimama na hajashuhudia ata mchezo mmoja.
"Kwa sasa kocha hawezi kuzungumzia lolote kuhusu ligi kuu na tumemtaka asifanye hivyo mpaka atakapoiongoza timu kwenye michezo mitatu ya ligi kuu.., hapo atakuwa na uwezo wa kusema lolote,” aliongezea kusema Tully.
Alisema kuwa kocha huyo ameiongoza Simba kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi na imemalizika kwa sasa nguvu zao wameelekeza kwenye michezo ya ligi kuu.
Akizungumzia mchezo wale, Kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, alisema kuwa kwa sasa akili na nguvu zao wamezilekeza kwenye michezo ya ligi kuu na wembe waliouonyesha kwenye michuano ya mapinduzi wanaelekeza kwenye ligi.
“Kwanza tunashukuru tunaingia kwenye ligi tukiwa na molali ya juu hasa baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la mapinduzi…, wachezaji wamepania kuelekeza nguvu zao kwenye ligi kuu na tunaanza na Ndanda kesho (leo),” alisema Matola.
Simba ambayo imetoka kutwaa kombe la mapinduzi inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi tisa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment