Na Albert G Sengo, Mwanza.
DIWANI wa Kata ya Nyamagana Jimbo la Nyamagana, Bikhu Kotecha leo amekabidhi mipira 10 na Kombe dogo kwa wafungwa na askari wa Gereza Kuu la Butimba lililopo Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.
Hatua hiyo ya Diwani Kotecha (CCM) kukabidhi mipira kunafatia ombi la viongozi wa wafungwa na mahabusu kupitia uongozi wa Gereza la Butimba ili kuwasaidia kuburudika, kuimalisha afya zao kupitia michezo na kudumisha mahusiano baina ya mahabusu na wafungwa na kuendeleza vipaji na ushabiki wa timu za Simba na Yanga na vilabu vingine vikiwemo vya Ulaya.
Kotecha akikabidhi alisema ametekeleza ahadi aliyoitoa mwaka jana alipowatembelea wafungwa hao katika ziara aliyoifanya akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa kiserikali hivyo ametekeleza ikiwa ni sehemu ya jamii ambayo inawajibu ya kushiriki na kuendeleza vipaji japokuwa wako chini ya utaratibu maalumu wa Gereza, Pia kutokana na mahusiano ambayo Kata yake imekuwa ikisaidiwa na wafungwa katika ujenzi wa miradi ya kijamii ikiwemo Sekondari ya Kata hiyo.
Mmoja wa viongozi wa wafungwa na mahabusu waliopo katika gereza hilo alimshukuru Diwani Kotecha kwa kuwakumbuka na kutekeleza ombi lao , kwa kueleza kuwa pamoja na kuwa gerezani kwa makosa mbalimbali bado ni sehemu ya jamii na inayohitaji kubadirika na kupata burudani ikiwemo ya soka na kulinda vipaji vyao kupitia timu tisa zilizopo ndani ya Gereza hilo zikiundwa na mahabusu na wafungwa.
Naye Mkuu wa Gereza la Butimba, ACP Jail Mwangunda , amepongeza utekelezaji wa ombi la watu ambao ni sehemu ya jamii wanaotumikia adhabu ya makosa mbalimbali lakini pia uamuzi wa Diwani Kotecha wa kuthubutu umeonyesha ungwana na upendo wa hali ya juu na kuonyesha mahusiano yake na uongozi wa Gereza hilo.
Msaada huo wa mipira kumi uliotolewa na kukabidhiwa na Diwani Kotecha kwa uongozi wa Gereza, wafungwa na mahabusu, ambapo viongozi wa wafungwa na mahabusu wamekabidhiwa mipira sita na kombe dogo watakaloshindania, timu ya askari wa Gereza hilo mipira miwili na timu ya askari ya wanawake mipira miwili ya netiboli.
CREDIT:SHAFFIHDAUDA
No comments:
Post a Comment