ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 5, 2015

HIKI NDICHO KIRUSI KINACHOITAFUNA SIMBA

Simba ni klabu kubwa sana katika historia ya soka nchini na Afrika Mashariki na Kati kiujumla. Hii haina ubishi kutokana na mafamikio yake katika soka miaka ya nyuma hadi ikafikia hatua ya kupachikwa jina la “TAIFA KUBWA”.

Simba ilikuwa tishio lakini kwa miaka ya hivi karibuni imegeuka na inaandamwa na matokeo mabovu.
Mwaka 2011-2012 Simba iliambulia nafasi ya 3 katika ligi ikiwa nyuma ya Yanga na Azam, msimu wa mwaka 2013-2014 ilishika nafasi ya 4 nyuma ya Azam, Yanga na Mbeya City iliyoingia kwa mara ya kwanza katika ligi.

Msimu huu wa 2014-2015 simba bado inaendelea kuchechemea kwani katika michezo yake 8 iliyocheza imejikuta ikitoka sare michezo 6, imeshinda 1 na kufungwa 1 na kujikusanyia jumla ya alama 9 ikiwa katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi (VPL)

Nini chanzo cha matokeo haya mabovu..?

Lawama zangu nazishusha kwa uongozi wa Simba chini ya rais ‪#‎Evance_Aveva‬ na makamu wake ‪#‎Geofrey_Nyange_Kaburu‬. Uongozi huu umesababisha makundi ndani ya klabu.

Leo hii kuna simba Ukawa ambao ndio wanalaumiwa kwa matokeo mabovu lakini uongozi umeshindwa kuketi na kutatua tofauti zao.

Viongozi wanawatukuza wageni na kuwapuuza wazawa. Nini thamani ya akina Mkude, Maguli, Singano, Isihaka na wengine wanaopigwa danadana kuhusu mishahara yao lakini bado wanajituma uwanjani..? Okwi amegeuka kuwa mfalme pale msimbazi, haudhurii mazoezi lakini kwenye mechi anapangwa tena na unahodha juu..

Wachezaji wa simba wagewanyika makundi makundi kutokana na upendeleo huu kwa Okwi wakati wengine wanapuuzwa. Ameaga kuwa anakwenda Uganda kwenye fungate na kuicha klabu ikifanya vibaya huko Zanzibar kumbe yupo humu humu Dar es salaam akiponda raha.

Wako wapi akina Simon Sserunkuma na Owino waliowatukuza lakini leo wametokomea kwao Uganda wakiiacha Simba ikifanya vibaya..?

Hans Pope ndio kila kitu pale msimbazi, analoamua ndilo linakuwa, alisema Kiemba ataondoka na kweli akang’oka. Akarudia Phiri anaondoka, japo Kaburu alipinga na kusisitiza kuwa bado ni kocha wa simba lakini mwishowe amendoka. Kulikuwa na haja gani ya kumuacha Tambwe aliyeisaidia simba msimu uliopita..? 
Amaa kweli hili ndilo soka la Bongo..!!
Credit: Shaffih Dauda.

No comments: