Advertisements

Thursday, January 29, 2015

Tanzania na China kuendeleza ushirikiano katika Maeneo Maalum ya Uwekezaji

Mkurugenzi wa Eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) nchini, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akizungumza na Bw. Li Xuhang, Naibu Mkuu wa masuala ya Siasa katika Ubalozi wa China hapa nchini kuhusu mikakati ya Serikali ya Tanzanania katika kuhamasisha uwekezaji nchini katika Maeneo Maalum na kuimarisha ushirikiano na Serikali ya China katika masuala ya uwekezaji kwenye Maeneo Maalum. Mazungumzo yao yalifanyika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Sehemu ya Wajumbe kutoka Ubalozi wa China hapa nchini waliofuatana na Bw. Li Xuhang. 
Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na EPZA wakifuatilia mazungumzo kati ya Kanali Mstaafu Simbakalia na Bw. Li Xuhang. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Nathaniel Kaaya, Bw. Lamau Mpolo (kushoto), Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo wa EPZA na Bw. Iman Njalikai (kulia), Afisa Mambo ya Nje. 
Mazungumzo yakiendelea 
Kanali Mstaafu Simbakalia akiwaeleza jambo Bw. Li na Afisa kutoka Ubalozi wa China mara baada ya mazungumzo yao. Picha na Reuben Mchome


No comments: