Advertisements

Monday, January 26, 2015

TASWIRA MBALIMBALI ZA TIGO MUSIC LILILOFAFANYIKA LEADERS CLUB

 Christian Bella akiwa jukwaani na bendi yake ya Malaika
 Malaika kazini...
 hawa ndio Yamoto Band...
 ..kama kawaida, Mkubwa na wanawe
Picha kwa hisani ya Mdimuz blog.
na kwa picha zaidi na maelezo bofya soma zaidi

 Nyomi lililokubali...
 Aslay katika mzuka wake
 Linah Sanga
 Shilole alikuja akiwa ameongeza dansa
 Salaam kwa mashabiki
 Raha sio rahaaaaaa?!!
 Agah....
 Ikaja zamu ya Vanessa Mdee
 Naye akapiga show yake vizuuuuuri
 Whats Up, whats up, what's Up...
 barnabas Classic alipanda jukwaani kumpa tafu Vee Money
 Juma.... a.k.a Juv
 Jamaa alishangiliwa sana huyu hasa baada ya kutambulishwa na vanessa
 Mzuka ukipanda, na hisia zikikubali?
 Young Dee
 Show yao ikaisha hv
 Malkia wa Uswazi, Sarah Kais
...Sugua gaagggaaaa....
 Jamaa alipiga show akiwa na furaha sana
 Kwa mara ya kwanza alikuja na madansa ambao ni raia wa kigeni
Dansi lilipigwa laivu jukwaani
 Sheji la Fud Q liliongozwa na Stamina kutoka Moro
Kisha Young Killer Msodoki
Kizazi kipya cha Hip Hop kwa upande wa akinadada nacho kilionesha umahiri wake
Ngosha na jeshi lake...
The heavy Weight naye...
Don Kolli na Jizzle
Shilole akaibuka tena kumpa tafu Jizzle katika Zali la mentali
Mitego katika kasri ya The |heavyweight
Yallah....
A City is in the Building Baby... WEUSI
Mstari kwa mstari..
 ...bila kukunja goti FA na AY?
...sijui muda ulikuwa unahusika? 
 Salama alikuja kutoa salamu jukwaani
 ...Kiba for real
 Platinumz
USIKU wa kuamkia juzi tamasha la Kiboko Yao lilifanyika katika viwanja vya Leaders Club na kuacha historia kwa mashabiki na wasanii wa muziki nchini.


Tamasha hilo lililoandaliwa na kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania, lilikuwa na lengo la  kuzindua muziki wa Tigo ujulikanao kama “Tigo Music” kwa kushirikiana na Deezer, ambayo ni huduma ya kimataifa inayorusha muziki,  itakayowapa wateja wake muziki usiokuwa na kikomo kutoka kwenye viganja vyao kupitia simu za mikononi.



Deezer umetajwa kuwa mpango utakaowapa nafasi wasanii wa hapa nchini kujiongezea kipato kutokana na nyimbo zao ambazo zitakuwa zimesikilizwa kupitia huduma hii. Wasanii watapewa mafunzo ya jinsi ya kutumia na kunufaika na huduma hiyo.



Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala akihutubia maelfu ya mashabiki kabla ya kuanza kwa tamasha hilo, aliyasihi makampuni ya mawasiliano kuwatendea haki wasanii katika ushirikiano wa kikazi baina yao ikiwamo kuwalipa kiwango kinachostahili katika miito ya simu.



“ Ni matumaini yangu uzinduzi huu utaweza kuwanufaisha wasanii wetu, pamoja na kuiingizia serikali pato litakalotokana na biashara baina yenu na wasanii hawa. Mna kila sababu kuhakikisha kwamba huduma hii inawanufaisha wanamuziki wetu moja kwa moja,” alisema Mukangara wakati wa uzinduzi huo.

Awali wanamuziki wa bendi kama Mashauzi Classic, Christian Bela na wengineo walipasha jukwaa, kabla ya kuwapisha viongozi mbalimbali kutoa nasaha zao na kuzindua rasmi promosheni hiyo.

Tamasha
DJ Mafuvu ndiye aliyepanda jukwaani na kuanza kupasha kabla ya washereheshaji wawili Sam Misago na Dullah hawajapanda jukwaani na nyimbo mbalimbali za wasanii wa zamani ambazo ziliwaamsha mashabiki. ‘Naja’ wimbo ulioimbwa na Juma Nature ndiyo uliozidi kuwavutia mashabiki na kuamsha shangwe na vifijo.


Ya Moto Band walipanda jukwaani na kuonyesha umahiri wao katika kuimba, huku wakitambulisha wimbo wao mpya ‘Nitakupwelepweta’ kabla ya kuwapisha wasanii wengine akiwamo Shaa, Linah, Ben Pol, Stamina, Young Killer, Fid Q, Profesa Jay, Vanessa Mdee, Mwana FA & AY, Barnabas, Shilole, Weusi na wengineo wengi.



Ben Pol ni kati ya wasanii waliofanya mabadiliko makubwa katika kuonyesha uwezo wao jukwaani, baada ya kupanda na madansa wawili ‘wazungu’ ambao walicheza vilivyo wakati akitumbuiza wimbo wake mpya ‘Sophia’.



Kwa upande wa Vanessa Mdee, kama kawaida yake alifanya shoo ya aina yake, lakini alionekana kuzidiwa baada ya sauti yake kushindwa kutoka ipasavyo, baada ya kujituma kwa kucheza alipokuwa jukwaani.


Mpambano Mkali
Wasanii waliokuwa wakisubiriwa ni Diamond Platnumz na Ali Kiba ambao hata hivyo ratiba zao kupanda jukwaani zilikuwa ni mwishoni. 


Ali Kiba alianza kutumbuiza kupitia wimbo wake wa zamani uliomtambulisha katika muziki mwaka 2007, ‘Cinderela’ na baadaye alimwaga nyimbo nyingi alizowahi kutamba nazo.



Wakati huo wote shangwe na vifijo zilisikika kutoka kwa mashabiki, ambao wengi wao walikuwa wamevalia fulana zenye jina la ‘Team Kiba’. Wakati wote wa shoo yake, kulikuwa na utulivu ambapo mashabiki waliongozwa na msanii huyo kuimba nyimbo zake zilizowahi kutamba.



Diamond Platnumz alipokea jukwaa kutoka kwa Ali Kiba ambapo alifanya shoo nzuri zaidi na pindi alipoanza kuimba, kuna baadhi ya mashabiki walianza kutupa chupa jukwaani zilizoaminika kwamba zilikuwa na mikojo, sambamba na mawe.



Nyota huyo hakujali na kuendelea kushusha burudani hadi mashabiki hao walipotulia. Diamond aliona isiwe shida, akaamua kuanza kufungua maburungutu ya fedha na kuzirusha kwa mashabiki noti za Sh10,000 ambapo walizipokea kwa mikono miwili na kuanza kumshangilia kana kwamba walisahau walichokifanya awali.



Baadhi ya mashabiki waliovalia fulana za ‘Team Kiba’ alionekana wakizigombea fedha hizo na baadaye waliendelea kumshangilia Diamond.



Vimbwanga

Katika hali isiyo ya kawaida msanii Ali Kiba alionekana akipita katika ukuta ‘aliruka ukuta’ majira ya saa 05:37 usiku wakati akiingia katika viwanja vya Leaders Club.


Licha ya kuwepo kwa milango miwili ya kuingilia upande wa VIP, kwa watu waliokuwa nyuma ya jukwaa, walimshuhudia akiingia kwa staili hiyo hali iliyowashangaza wasanii wenzake na watu waliokuwa wakifanya shughuli mbalimbali nyuma ya jukwaa hilo.



Kilichowashangaza wakongwe wa muziki ni Ali Kiba kuwapita bila kuwasalimia, ambapo asilimia kubwa ya wasanii walilalamika kitendo cha yeye kushindwa kuwasalimia wenzake. Licha ya kufanya shoo nzuri,

Ali Kiba bado amewaachia wasanii wenzake maswali mengi.


Gereza la Leaders Club

Baadhi ya vijana usiku wa kuamkia jana walijikuta wakilala katika gereza dogo ndani ya tingatinga la polisi, lililokuwa limepaki katika lango kuu la kuingilia viwanja hivyo.
Ulinzi uliimarishwa vilivyo na yeyote aliyekamatwa na kosa, alifungiwa humo kwa muda usiopungua saa tatu na baadaye aliachiwa huru na kuombwa asionekane kabisa ndani ya eneo hilo.

No comments: