Kwa mujibu wa Gazeti la Marokocho, mwanamziki na mwigizaji wa filamu hapa Bongo, Zuwena Mohammed “Shilole” alimpiga kofi mchuma wake Nuh Mziwanda mbele ya umati wa watu. Gazati la Makolokocho liliripoti kama ifuatavyo;
Jumamosi iliyopita ndani ya Tamasha la Kiboko yao lililofanyika Leaders Club, ilishuhudiwa live Msanii Shilole akimchezeshea kichapo mchumba wake Nuh Mziwanda kwa madai kuwa Nuh alikua hataki kuondoka nae eneo la tukio, mchekeshaji Steve Nyerere alijitokeza kuamulia ugomvi na kufanikiwa kumtoa Shilole eneo lile lakini baada ya muda Shilole akarudi na kumdai funguo ya gari Nuh ambaye siku hiyo alionekana kuwa mpole ikabidi mabaunsa waingilie kati na kumtoa kwa nguvu shilole, baadae Nuh alionekana akitoa machozi na Malkia wa Taarabu Khadija Kopa alionekana akim'bembeleza na kumfuta machozi.
Hili swala la wanamke kutembeza kichapo kwa wanaume zao linazidi kukua kwa kasi napendekeza wanaume nao waunde chama chao cha kuwatetea...
6 comments:
tatizo vijana wengi wako "keept men'wanawekwa wanahudumiwa na kupea pesa pocket money badala ya wao kuwatunza mademu sasa wao wanatunzwa unatarajia nini hapo,uanamume wako uko wapi ewee kijana mwanamme.wewe ndo kichwa cha familia mungu kakumba uwe mkuu utawale kwa motto wa kike leo hii wewe umejigeuza unataka kutunzwa. heshima unadhani itatoka wapi.
wako wavivu sana vijana wengi wa kiume hawataki kujituma wanapenda short cut katika maisha mwisho wa siku wana kuwa "keept men".
wache wazabwe vibao na wanawake na nawaambia wanawake nao wawateme mate because umejizaraulisha mwenyewe.
Thubutu dume la mbegu,baro baro unakazi yako hata kama mpiga box unarudi nyumbani unalipa bill zako fresh unamhudumia mummy ndani na watoto thubutu demu akufanyie ujinga huu,jiulize kwa nini,umejipa heshima mwenyewe unajivika mwenyewe unajihudumia mwenyewe na yeye wife pia na watoto heshima tosha hapo mwanamke hakuchezi hata kidogo hapo.
akikutazama anakuona kifaa simba wake,mlimzi wake ujinga hawezi kukufanyia labda mwanamke kapata wazimu na hautibiki.
jiheshimuni wanaume wenzangu msiwe wavivu jitumeni kuna siku mta pata utajiri wekeni heshimi kwa kuwa na kazi hata kama kupiga box ndo uwanaume huu,usiruhusu mwenya mwanamke akuhudumiye kaa mtoto wa kike mwisho wa siku atakudharau tu.
by nature a man is a giver not a taker.usibweteke kijinga kwa mali ya demu ukawa mtumwa wake.
anaitaaaa.
Mimi sikubalianani na wewe hapo juu hayo ni mawazo ya kizamani na kishamba. Jukumu la mwanaume ni kumpa mapenzi mwanamke wake na kumtosheleza hata vitabu vya dini vimeandika hili. Haijalishi ni nani analeta pesa nyumbani. Kuna mwanaume hasa bongo wanamwaga mapesa kwa wanawake zao na vitu vya dhamani matokeo yake wanawake wanatoka nje sasa lini ni fedheha hapa kupigwa kofi ama hili? pia unabidi kustaarabika mwanamke wako akikupiga kofi utakiwi kurudisha, kuna msemo tena wa zamani kuwa mwanamke upigwa kwa upande wa kanga tafakari maana yake.mwisho hauna ushaidi wowote kumpiga ni kumdhalilisha labda ni ishara ya mapenzi ni katika jitihada za kuimalisha mapenzi yao
bro umemaliza kila kitu hapo.
tena siku hizi wako wengi sana ma brother man, ma younky dude wanaopenda kula pesa za wanawake,wanajibwetega bwete ovyooo.wanatia kinyaa kwenye jamii ya wanaumme.
mwanamme jembe na jembe lazima liheshimiwe hakuna mawazo ya kizamani wala nini,unapigwa kofi hata mama yako hawezi kukupiga kofi,si semi kwamba ukipigwa kofi na wewe umrudishiye, no and no utamumiza.mwanamke anapigwa kwa kanga ni kweli but kupigwa kofi hadharani kwanini umejenga mazingira hayo?akudharau hivyo, lazima utakuwa unamtegemea sana huyu mwanamke. Dume zime kweli Unalala katika nyumba yake,Anakuvishe,anakulishe,anakupa pesa na gari lake unalitumia na kutamba nalo kwa mademu wenginewe bila ya yeye kujua na kujifanya kokorikoo wakati ngangaharika
its such a shame mwanamme mtu mzima umebweteka unasubiri mtoto wakike achume aje alete wewe kazi kubwa uliyonayo rasli mali namtaji wako ni kiuno chako.
zuga zuga nenda ferry lete hata vidagaa au chajoo mchicha ulete nyumbani weeki mara mmoja,kama huna kitu mfukoni.
unajidhalilishaaaa mwenyewe ukibweteka mwisho wa siku matokeo ndo hayo ya kupigwa makofi kama mtoto wa kambo.
najua wanaume wanaopenda kubweteka wako wengi watoto wamama bado watatete sana UTAWAJUA KWA MATUNDA YAO.
MWANAMME PESA TAFUTA UTAIPATA MUNGU WA WATU WOTE NA SI WA OTHMAN PEKE YAKE.
MWANAMME JEMBE FAHARI YA WAZAZI NA JAMII KWA JUMLA.USIVUWE FAHARI YAKO KWA KUJIFANYA SHARO UHAROOO.
KUWA KIDUME DUME (BARO BARO) WA KWELI KWELI.DEMU ATAKUPA HESHIMA YAKO.
MWANAMME KUHESHIMIKA SI KUBEBA HANDBAG ZA DEMU WAKO NA KUVAA SURUALI ZAKUSHUKA MAKALIONI NA VIHERENI VYA PUA NA MASIKIONI.
MWAMME PESAAA NA HESHIMAA YAKO ILINDEEEEEEEEEEEEEE.
Anonymous wa 1:1 pm eti umesema mwanamme akipigwana demu wake ni ishara ya mapenzi na katika jitihada za kuimarisha mapenzi yao?
yani wewe mwisho mwanzo ebwana weee so wewe utakuwa unakubali kupiga vibao mbele za njemba wenzako hadharani ?
aiseee si dhani kama hii comment kaandika mwanamme,siamini na sitaki kuamini hivyo lakini kama wewe ni mwanamme kweli yani sina la kusema
nadhani bado mdogo,mwanamme mtu mzima hawezi kukubali kuvunjiwa heshima yake ovyo ovyo namna hivi na si ubaba ila sijaonaga.
nadhani bado wewe kinda.
nawakilisha
Aaaah !!Badhi ya wanawake wanapenda design za wanaumme kama hawa; damu mbichi mbichi,utasikiya wenyewe wanakuambia, handsome boy wangu,he is so cute and so fine, anatembea naye barabarani kwa madoido utadhani gari la abeid limekata spring.
wanatuacha sisi wenye heshima zetu waache mashuga mummy wadhalilike wenyewe.
Post a Comment