WAFUASI 29 kati ya 30 waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam wameachiwa leo baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Wafuasi hao walikamatwa majuzi huko Mtoni Mtongani, Dar wakati Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akielekea Mbagala kuwataka wananchi watawanyike baada ya maandamano ya chama hicho kuzuiliwa na jeshi la polisi.
Wafuasi hao 29 wameachiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar baada ya kila mmoja wao kutimiza masharti ya dhamana kwa kutoa kiasi cha shilingi 100,000 pamoja na barua ya mdhamini mmoja ambaye hana hatia.
Mpaka mwandishi wa GPL anatoka eneo hilo la mahakama, mmoja wa watuhumiwa alikuwa bado mikononi mwa polisi kwa kutokamilisha taratibu za dhamana hiyo akiendelea kumsubiri mdhamini wake aliyechelewesha barua ya udhamini.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amesema kesi yao itatajwa tena Februari 12, 2015.
kusikiliza kesi baada ya kupewa dhamana.…
WAFUASI 29 kati ya 30 wa CUF waliokamatwa kwenye jaribio la maandamano ya kuwakumbuka wafuasi wenzao waliouawa mwaka 2001, Mbagala-Zakhem jijini Dar sanjari na mwenyekiti wao, Prof. Ibrahim Lipumba, mchana huu wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wafuasi hao wameachiwa leo kwa dhamana baada mwenyekiti wao kupandishwa kizimbani juzi katika Mahakama Kisutu kujibu kesi ya kuhamisisha wafuasi wa chama hicho kutenda kosa la jinai kuhamasisha maandamano Januari 27, mwaka huu.
Wafuasi hao 29 walikidhi vigezo vya udhamini na kuachiwa lakini mwenzao mmoja ambaye aliendelea kushikiliwa hadi pale baada ya mdhamini wake kuchelewa kutimiza masharti ya dhamana.
Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru alisema shauri hilo litasikikilizwa tena Februari 12, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment