ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 2, 2015

WALIOTAKA KWENDA IKULU WAISHIA RUMANDE DAR

VIJANA watatu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, wamekamatwa na polisi eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 2, 2014, baada ya jaribio lao la kufanya matembezi kutoka mkoa wa Geita wakielekea Ikulu ya Dar es Salaam kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha malalamiko yao. Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, vijana hao watatu, Juma Maganga, Khalifa Selemani na Athanas Michael, walielekezwa na maafisa usalama kumuona yeye DC baada ya kuwasili kwenye eneo lake la utawala wakitokea Geita, ili awape baraka za kwenda Ikulu. Lakini walipofika ofisini hapo, DC huyo alitaka kujua nini hasa kilichowafanya watembee safari ndefu kama hiyo? DC Rugimbana alisema, walimweleza kuwa Mosi, Wanataka Kumnuona Rais ili wamueleze kuchukizwa kwao na vitendo vya viongozi kula rushwa na hakuna hatua dhabiti zinazochukuliwa dhidi yao, kukithiri kw amatumizi mabaya ya rasilimali za taifa, kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia, na kudai kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika. Baada ya kusikia hayo, DC aliwaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kumuona Rais wa nchi, hata hivyo sio kumuona kiholela bali ni kwa utaratibu maalum, na kwa kufikia hatua waliyofikia vijana hao, tayari walikuwa wamevunja sheria lakini akawataka wasubiri awasiliane na wakubwa ili waandaliwe utaratibu wa kumuona Rais. Hata hivyo vijana hao walikataa na walipotoka nje ya ofisi ya DC hapo Kinondoni, walifanya tena jaribio la kuelekea Ikulu na safari hii polisi hawakufanya masihara, waliwaweka chini ya ulinzi mita chache kutoka taa za kuongozea magari kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa ukiwa uneelekea Kariakoo.
Vijana hao wakiwa kwenye safari yao eneo la Magomeni Kagera
Vijana hao wakiwa chini ya ulinzi wa polisi wakielekea kituo cha polisi Magomeni Mapipa
Polisi wa kutuliza ghasia akiwahi sehemu walikoelekea vijana hao tayari kuwakamata
Polisi wakionye raia kutounga "tela" safari ya vijana hao wakati wakiwa eleo la Magomeni Mwembechai
Polisi wakimdhibiti mmoja w avijana wasiokubali "kupitwa"
Polisi wakiwahi kukamata vijana
Vijana wakiwa chini ya ulinzi
Wakionyesha mshikamani baada ya kukamatwa
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, akiwaeleza waandishi wa habari matokeo ya mazungumzo yake na vijana hao Picha kwa hisani ya K-Vis

12 comments:

Anonymous said...

Asanteni Tanganyika Tanganyika nakupenda kwa Moyo wangu wote...

Anonymous said...

That's what we call true patriotism. Big up young men.

imrom92@hotmail.com said...
This comment has been removed by the author.
Anonymous said...

Jina la mkuu wa hii wilaya aliyejipendekeza kwa kuwakamata raia wasio na kosa linafanana na wale wanaotoka kule kule walikogawana mapesa ya ESCROW. Hivyo kwa vile moja ya ajenda ya vijana hao ni kupinga ufisadi, mkuu huyo wa wilaya akaona ndugu zake wanaenda kuchongewa zaidi. Tanzania ni nchi huru na kila mmoja ana haki ya kutembea anakotaka kutembea.

Anonymous said...

Hali ya maisha Jamani imekuwa nguvu sanaana,,kwa mtazamo wangu hawa vijana wangesikilizwa na polisi badala ya kuuza sura, waende wakawashughulikie panya-road gangs.hawa panya road wanaleta maafa makubwa sana,,wanabaka,,wanajeruhi,,wanapora. Sasa tunapoteza muda kuuza sura kwa vijana hawa watatu waliotembea Kutoka Geita kwa mguu wakiwa na bendera ya chama tawala.

Anonymous said...

Mpaka hapo sijaona sheria ambayo vijana hawa wameivunja. Sana sana ni kwa viongozi wetu kutumia vibaya vyombo vyetu vya dola. Wangekuwa wamevunja sheria kama wangefika kwenye lango la Ikulu na kutaka kuingia kwa nguvu, bila kibali cha security officers wa Ikulu.

Anonymous said...

Madai yao yote ni sahihi na yakitokea Tanzania kwa miaka nenda rudi. Ila kwa kuwa-wezi hao ni swahiba wa serikali, kuchukuliwa hatua imekuwa ni mfano wa njozi ya abunuwasi. Itabidi wananchi waanze kuishinikiza serikali kuwachukulia hatua stahili hawa watu waotumia madaraka kinyume cha sheria.

Unknown said...

Vyama vya upinzani viko wapi???? Huu ndo muda mzuri wa kujitolea mhanga na kuwatetea hawa vijana... Upinzani hamna Tanzania!!

Anonymous said...

Tanzania tushakuwa nchi ya dikteta olewko utamke vibaya hadharani dhidi ya raisi au mafisadi wake

Anonymous said...

Tanzania hakuna upinzani wa dhati bali ni upinzani maslahi. Usitegemee Ukawa kuwaunga mkono hawa vijana na sababu kubwa hawana maslahi. Ukawa huibua issues/skendo ambazo zitawawezesha kuitwa pembeni na kupoozwa ili yaishe..

Anonymous said...

Siku zina hesabika taratibu mboga imesha zidi chumvi..

Anonymous said...

wote hapo juu mliotoa comment zenu nakupeni kumi,ni wazalendo halisi lets keep on moving like this, tuwaonyeshe wakuu wetu sisi si wajinga na si wakupewa vijisenti mbuzi vyakufungwa midomo yetu.


watanganyika wameshaamka mwaka huu enyi ukoo wa panya msidhani bado watanganyika wajingaaaaaaaaa.