Advertisements

Thursday, January 8, 2015

YANGA NAYO OUT KOMBE LA MAPINDUZI YAPIGWA 1-0 NA JKU

Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe, akiwa chini akijilaumu baada ya kukosa bao la wazi katika mchezo wa Robo fainali ya Kombe la Mapinduzi uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Aman mjini Zanzibar. Katika mchezo huo JKU ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Amour Omary katika dakika ya 72.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga ni timu ya tatu kuaga mashindano hayo ikiungana na Azam Fc, iliyofungwa na Mtibwa Sugar na Kcc iliyofungwa na Polisi, ambapo sasa JKU itakutana na Mtibwa Sugar katika hatua ya Nusu Fainali.

No comments: