ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 20, 2015

YANGA SASA WATAKA WANAJESHI WACHEZE LIGI KUU YAO

Uongozi wa klabu ya Yanga umeshauri timu za majeshi kupewa nafasi ya kushiriki Ligi Kuu Bara ya wanajeshi.
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe (kushoto) akiwa amekabwa roba na mchezaji…
Msemaji na mkuu wa kitengo cha Yanga, Jerry Muro amesema timu za majeshi zimekuwa zikigeusa mchezo wa soka kama vita.
"Kweli ile ni vita na si jambo jema. Hivyo tunawaomba kama TFF wataweza basi wawape nafasi watu hawa kucheza ligi yao.
"Wacheze timu za majeshi maana wao watakuwa wana mbinu za kijeshi kupambana. Sisi raia hatuwezi, wanaweza wakatuua," alisema Muro.
"Ukiangalia tukio la yule beki wa Ruvu Shooting akimkaba Tambwe utagundua hakuna tena uungwana katika soka."
Picha iliyochapishwa katika gazeti bora la michezo la CHAMPIONI imezua gumzo kubwa katika mitandao mbalimbali nchini.
Picha hiyo inamuonyesha beki George Michael akimkaba Tambwe kikatili huku akiwa anavuja damu mdomoni.

1 comment:

Anonymous said...

Hawa wanajeshi hawana adabu ni wapuuzi waondolewe kwenye ligi ya watu wenye akili. Sijui watakuwa lini, na referee anaogopa atapigwa, kweli sijui kama nchi tunaelekea wapi? Mimi siyo mpenzi wa Soca lakini kitendo cha huyo mchezaji wa Ruvu JKT kumpiga na kumtolea maneno ya kashfa kuwa kwao wanapigana na yeye ni mkimbizi.....HAYA NI MANENO YA KASHFA KUTOLEWA NA ALIYETOA ANA MATATIZO YA KIAKILI.