ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 10, 2015

ASYA IDAROUS AZUNGUMZA NA WANAHABARI

ASYA IDAROUS AZUNGUMZA NA WANAHABARI
Katikati ni Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsin

Asiya Idarous Khamsin Fabak Fashions ikishirikiana na Fashion news Tanzania inawaletea Lady in Red 2015, katika ukumbi wa Mog Bar ( Nyumbani Lounge) siku ya Ijumaa Tarehe 13 february 2015 usiku wa kuamkia Vallentine Day kwa kiingilio cha buku kumi aka 10000 na VIP 20000 ni kwaanzia saa 2 usiku.
Leo Asya na timuyake ya maandalizi ya Lady in Red 2015 wamekutana na wanahabari Mog Bar na kuzungumzia mwenendo mzima wa Show hiyo kubwa ya kipekee ambayo hufanyika kila mwaka kwa kukuza ubunifu wa mitindo ya nguo hapa nchini.

Aidha kufuatia mkutano huo Asya alisema kuwa ” Lady in Red itafanyikia hapa Mog Bar ( Nyumbani Lounge) kwasababu ilikuwa ifanyikie ‘Coco beach hall’ lakini kumeona ni vyema tuiweke kwenye sehemu yenye uwezekano wa usafiri kwa wapenzi wa mitindo na Fashion hapaTanzania, katika show hiyo, Mh.Shyrose Bhanji Mbunge wa Africa Mashariki ndiye atakaye kuwa mgeni rasmi kwenye Fashion Show ya Lady in Red” pia Asya aliongeza kuwa “siku hiyo kutakuwa na burudani nyingi kama Gusa Gusa Mim band, Traditional Dancer pia kutakuwa na mitindo mbalimbali ya nguo nyekundu kutoka kwa wabunifu tofauti tofauti wa hapa Tanzania.
Imedhaminiwa na Maji poa, Darling Hair, Vayle Spring, Eventlight, Voice of America Mog Bar, Jmbo leo, Sibuka Tv Chanell Ten, Michuzi, Media, Haak neel Production, Baker Desighs nk. (picha na Victor Petro)

No comments: