Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja ya Nchini Marekani Dr. Robert Shumake akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake iliyopo katika Jengo la Msekwa ndani ya Viunga vya Bunge la Jamuhuri nya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja ya Nchini Marekani Dr. Robert Shumake Bungeni Mjini Dodoma.(Picha na – OPMR)
Na Othman Khamis. OMPR
Kampuni ya Ms Shimoja yenye Makao Makuu yake katika Jimbo la Michigan Nchini Marekani iko mbioni kutaka kuanzisha kituo cha Matangazo ya Televisheni Mjini Dar es salaam Nchini Tanzania kitakachotoa huduma ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki.Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ambae pia ni Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani Dr. Robert Shumake alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake katika Jengo la Msekwa ndani ya viunga vya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Dr. Shumake alisema licha ya kwamba matangazo ya Televisheni yanachukuwa sehemu kubwa ya burdani lakini Kituo hicho kitalenga zaidi kutoa vipindi wa Elimu vitakavyowasaidia wananchi na hasa wanafunzi wa elimu ya msingi, sekondari na vyuo vikuu Afrika Mashariki.
Alisema mipango inaandaliwa na Kampuni hiyo katika kuyashirikisha Makampuni ya Mitandao ya Mawasiliano Duniani ya Google na Microsoft ili kuona Elimu inayokusudiwa kufikishwa kwa umma kupitia matangazo ya Kituo hicho yanafanikiwa kwa kiwango kikubwa.


No comments:
Post a Comment