ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 6, 2015

Mke wa Rais wa Ujerumani Bi Daniela Schadt Afungua Skuli Mwera.

Jengo la Skuli ya Herrnhuter Academy School, ilioko katika Kijiji cha Mwera Wilaya ya Kati Unguja, iliofunguliwa na Mke wa Rais wa Ujerumani wakati wa ziara yake Zanzibar.
Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii Vijana na Wanawake Zanzibar Mhe Zainab Omar Mohammed, wakiwasili katika viwanja vya Skuli ya Herrnhuter Academy School, ilioko Mwera Wilaya ya Kati Unguja, kwa ajili ya ufunguzi wa skuli hiyo.
Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt, akifungwa Ua na wanafunzi wa Skuli hiyo baada ya kuwasili katika hafla ya ufunguzi wa majengo ya Skuli hiyo mwera Zanzibar
Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt, akiongea na Viongozi wa Kanisa la Monrovia Zanzibar baada ya kuwasili katika viwanja vya Skuli hiyo kwa ajili ya ufunguzi wake. alipofika Zanzibar kwa ziara ya siku moja na Mumewe Rais wa Ujerumani.
Mke wa Rais wa Ujerumani Bi.Daniela Schadt, akisalimiana na Viongozi wa Kanisa la Monrovia inayomiliki Skuli hiyo, alipowasili katika viwanja vya skuli hiyo kwa ajili ya ufunguza wa skuli hiyo mwera.

No comments: