ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 12, 2015

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe, Liberata Mulamula aanda chakula cha jioni kwa baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao kwa ukanda wa Afrika Mashariki nyumbani kwake

Balozi wa Ethiopia nchini Marekani na mwenyekiti wa mabalozi wa kanda ya Afrika Mashariki Mhe, Girma Birru akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa Balozi, Mhe Liberata Mulamula.

Balozi wa Uganda nchini Marekani Oliver Wonekha ambaye ni mmoja  wa mabalozi kutoka kanda ya Afrika Mashariki akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa Balozi. Mhe  Liberata Mulamula.
Balozi wa  Burundi nchini Marekani Mhe, Ernest Ndabashinze akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa Balozi Mhe, Liberata Mulamula.
Balozi wa  Kenya nchini Marekani Mhe, Robinson Githae akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa  Balozi Mhe, Liberata Mulamula. 
 Balozi wa Rwanda nchini Marekani Mhe, Mathilde Mukantabana  akisaini kitabu cha wageni nyumbani kwa  Balozi Mhe, Liberata Mulamula. 
Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula akiwakaribisha wageni waalikwa mabalozi waliofika nyumbani kwake kwa hafla fupi, baadhi ya mabalozi mfano Burundi na Kenya walisindikizwa na wake zao.
 Baadhi ya Maafisa wa ubalozi wetu waliombata na Balozi kwenye hafla hiyo, kulia ni Afisa Paul Mwafongo, akifuatiwa na Dr, Switbert Mkama pamoja na mwambata wa jeshi Kanali Adolph Mutta.
Mabalozi wakijiandaa kupata chakula cha jioni nyumbani kwa Mhe,balozi Liberata Mulamula ambaye ndio mwenyeji wao kwa jioni hio. 
Balozi Liberata Mulamula akiwa na furaha  kwani wageni wote waliweza kufika na kujumuika nae, pichani akiwa na mke wa balozi wa Burundi Madam Marie-Gloriose Kankindi aliyekua ameambatana na mumewe.

Mabalozi wakiagana na kumshukuru mwenyeji wao  Balozi Liberata Mulamula kwa hafla iliyofanyika kwa ufanisi mkubwa mno pichani ni mke wa Balozi wa Kenya nchini Marekani Madam Alice Wanjiku Njeri akijiandaa kuondoka.
                            PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.

1 comment:

Anonymous said...

Hongera sana Mhe. Balozi L. Mulamula kwa ukarimu wako, MUNGU akubariki sana.