
Nilisema baadhi ya watu wanajulikana kuwa, hawakai mbali na simu hata kwa dakika mbili, sasa ikitokea mwenza wake anapiga hapokei anajua anafanya makusudi kwa vile inaaminika hawezi kuwa mbali na simu kwa muda mrefu.
Nilizungumza na watu mbalimbali kuhusu mada hii ambapo mama Salama, mkazi wa Sinza D jijini Dar yeye alisema:
Niliwahi kugombana na mume wangu, nilimpigia simu ikaita wee mpaka ikakatika. Halafu ikapita nusu saa hajapiga wakati najua si kawaida yake kuwa mbali na simu.
DHANA YA DHARAU
Wengi niliobahatika kuzungumza nao walionesha kukerwa sana na tabia ya wenza wao kutopokea simu wakati ikiita wakiamini ni ishara ya kudharauliwa.
Afadhali simu isiwe hewani naweza kusema labda imejizima kwa bahati mbaya lakini kutopokea ni ishara kwamba ananidharau. Tena kama mimi huwa naamini mwenzangu hapo alipo anamwambia aliye naye, huyu naye kwa kusumbua kupiga simu. Hii huwa inaniuma sana, anasema Salim baba Malick, mkazi wa Msewe-Ubungo, Dar.
SIMU KUZIMA INALETA MATUMAINI
Francis Bekambo, mkazi wa Kigamboni yeye alisema ilitokea siku moja alimpigia simu mkewe akawa hapatikani. Alishangaa sana kwa sababu si kawaida yake.
Anasema: Lakini nikiwa nyumbani akaingia baada ya saa moja tangu nimpigie. Nilipomuuliza akaitoa simu kwenye begi na kugundua ilizima yenyewe kumbe ndiyo maana hakuwa hewani. Kidogo ilileta ukweli kuliko kama ningempigia halafu ikaita asipokee.
SMART PHONE NDIYO KABISAA
Kuna simu za kisasa smart phone ambapo mmiliki anakuwa na uwezo wa kujiunga na mitandao ya kijamii kama Instagram, Face Book au WhatsApp.
Imefika mahali simu hizi zimekuwa zikiibua migogoro kwa wapendanao kwa sababu kama WhatsApp mtu ana uwezo wa kujua mwenza wake yupo online au mara ya mwisho aliingia muda gani.
Mbaya zaidi, simu hizo za smart phone kwa kutumia mtandao kama WhatsApp mtu anaweza kujua upande wa pili unaandika sasa. Hali hiyo imezidi kuibua migogoro kwa vile mwenza anajua meseji yake imeshaonekana au simu imeshikwa wakati anapiga, sasa kwa nini usipokee?
MBONA HUPOKEI SIMU YANGU NAYO INAPOTEZA MUDA
Wakati huohuo kuna jambo lingine ambalo huwa linatokea na kusababisha wawili kupoteana Kiswahili. Utakuta mtu anapigiwa simu, mfano, mke anampigia simu mume wake, hakupokelewa. Baadaye anapiga tena, inapokelewa, palepale mke anaanza:
Mbona napiga simu hupokei?
Maneno haya yanapoteza muda bure kwani kama simu isingepokelewa mgeongeaje sasa? Kama simu haikupokelewa mwanzo sasa imepokelewa nenda moja kwa moja kwenye hoja au sababu ya kupiga.
USHAURI WANGU
Ushauri wangu kwa wote wenye wenza wao ni kwamba, waache kutumia simu vibaya. Kama umepigiwa halafu hukupokea labda uko taiti, haraka sana jitahidi ukimaliza utaiti wako mpigie mwenza wako ili kumuondoa wasiwasi kama siyo hofu.
Kwa wale ambao simu huzima bila kujua pia kunatakiwa kuangaliwa upya kwani kama wewe ni mtu wa kupigiwa simu mara kwa mara lazima ujiulize kwa nini simu yako haijaita muda mrefu? Lakini katika yote, wengi wameonekana kusema kuwa afadhali mwenza wake asiwe hewani kuliko kutopokea simu!! Chao!
GPL
No comments:
Post a Comment