ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 12, 2015

Diamond Platnumz 'Baba mtarajiwa' aanza kukusanya midoli ya mwanae kuchezea!

Diamond Platnumz kama mwanaume yeyote yule anayetarajia kuwa baba kwa mara ya kwanza tena kupitia mwanamke ampendaye, amepania vilivyo kumkaribisha mwanae kwenye sayari ya dunia.
Staa huyo ambaye hivi karibuni alikuwa nchini India, amepost picha akiwa supermarket kununua midoli kadhaa kwaajili ya mwanae huyo ajaye.
“Ushamba huu, eti nimeshaanza kununua vitoy vya kuchezea,” ameandika Diamond kwenye picha hiyo.

6 comments:

Anonymous said...

siyo ushamba baba fanya uwezalo ndo mtoto wako wa mwanzo na ulikuwa unahamu sana na mtoto so mungu kakubariki ndoa je vivi hapo baba?
unajua wewe mtoto wa kiislamu na zarinna pia so msiwe waislamu jina tuu, uzinzi unakemewa sana katika dini,mtoto angezaliwa katika uana halali.

cha muhimu uwe baba mzuri uche ubishoo sasa,ili mtoto umlee vizuri na muelekeo mwema

mtoto si midoli tuu but malezi mema yako umpe na mtoto anakuangalia wewe ndo kioo chake si utakavyo mkataza,akiuona wewe unafanya yasio na maana na ukimkataza hatokatazika anakutizama matendo yako.

tunakutakia kila la kheir na Baraka tele sema unatakiwa uwe baba mzuri baba mwerevu ukuwe sasa mambo ya kitoto toto umuache mtoto sasa okay.

hongera kwa kupiga ngoma yako vizuri na zarinna kuipokea.

Anonymous said...

zarinna bora umshikiliye this dude ashipepese macho yake popote zaidi ya kwako.

na bora hasa mamake wema amefurahi umempata zari,kwa sababu alikuwa anamtakia mema mwanawe,mwanamme aliyetulia si kicheche.

Anonymous said...

Acha ubishoo usidhani kupata mtoto ndio basi kuna kulea, na tunavyokujua tutakusikia vinginevyo baada ya miezi kadahaa! wako wengi pembezoni wanasubiria kukuchuna na mwenyewe mchunwaji unatarajia nini kuwa mtulivu acha mawenge!!

Unknown said...

mla makombo huyo.. unazaa na jimama lina watt watatu?? kijana una hela na kila kitu?? utakua umerogwa wewe.. wanawake wabichi wazuri wa kibongo.Jiandae kufilisika.feeeeewwwww

Anonymous said...

majimama ndo wanaojua shughuli hao wabichi vikojozi tu,majimama ndo anajua kila style na ana experience ya maisha hadanganyiki kwa punje ya mtama hao wabichi viruka njia akiona kibuzi anazaidi ya mumeo atataka kukipata cha huyo jamaa wa pembeni hajui kama ameazima au vipi.

majimama wanajua maisha wewe.na wastahamilivu wewe ukitaka maisha yakuende vizuri chagua majimama.

kwani alizaliwa nazo si amekuja akazichuma na akirudi kaburini atakwenda nazo achaa wewe kuwakashifu majimama.

kwanza mtoto mwenyewe kifaa huwezi hata siku mmoja kutia pua yako na kumtongoza zari wewe.

diamond usisikiye ya wakosaji wewe unaumiiki mzigo huo nenda nao kishakukubalia kukuzalia wewe nenda naye bega kwa bega mwangu

mungu akubariki sana muishi kwa raha wasipenda kuona unafurahi na zari wako wajinyoge wale sumu wakafiye mbele huko.

usiyasikilize maneno ya wakosaji hawakosi la kusema. wanatamani wangekuwa nafasi yako ila ndo hivyo basi. achana nao umewafunika vibaya sana na kupata toto na zari mtoto wa kweli.

kwa wale wote waliomsema diamond hazai sasa kiko wapi tusubiriye tu azaae na ningekuwa mimi wala nisingetangaza hii mimba ya mpenzi wangu ningesubiri mpaka katumbo kakubwa kakubwa na anazaaa,huwezi jua wabaya wako wengi wasije wakamfanyia kitu mbaya na asizae.

so next time watch out my dude.
please.

mdau anayekutakia mema diamond na zari always.

Anonymous said...

Diamond chunga sana unapo mnunulia mwanao midoli(wanasesere)usidhani ni ushirikina bwana mdogo ohoo.soma hapo china mambo yapo haya bwana.

Baada ya biashara ya mitumba kuruhusiwa hapa nchini, wafanyabiashara wamekuwa wakiingiza kila aina ya nguo na vyombo vya aina mbalimbali.

Moja wapo ya bidhaa ambayo inaingizwa kwa wingi nchini ni wanasesere (midoli) zikiwa katika maumbo mbalimbali kama magari, mbwa, paka, watoto, nyoka, chura nk.

Shetani akisaidiwa na wachawi wa nchi siku zote huwa wanatafuta milango ya kuingilia ndani ya maisha ya mtu, mara nyingi wachawi na majini huwa wanavaa maumbo ya panya, paka, mbu, nzi, mjusi kafiri kuingia kwenye makazi ya watu na kuwafanyia ulozi.

Siku hizi baada ya watu wengi kununua na kumiliki madoli, utakuta chumba cha mapumziko kimepabwa kwa madoli aina mbali mbali, kama wana watoto, utakuta chumba cha kulala watoto kimejazwa madoli, watoto wakicheza nayo. Magari nayo yamekuwa yakipambwa kwa midoli ya kila aina.

Wachawi wa nchi wakiingia ndani ya nyumba yako, wanachofanya ni kuweka majini yao ndani ya hiyo midoli au midoli sasa hivi ndiyo makazi ya wachawi na majini ndani ya nyumba yako, ndiyo maana tangu ununue hiyo midoli maradhi ya ajabu hayaishi nyumbani kwako.

Huu ni ushauri wa BURE kwa yeyote mwenye kuwa na sikio la kusikia na asikie, mwenye macho ya kusoma na akasoma hii habari na kuielewa, ataamua mwenyewe linalokupasa kutenda.