ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 5, 2015

KIKAO CHA KWANZA CHA BODI YA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI GEREZA KIGONGONI - BAGAMOYO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (aliyesimama) akitoa utambulisho kwa wajumbe wapya wa Bodi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu akitoa maelezo mafupi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Green Park iliyoko Bagamoyo.
Wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji kutoka Jeshi la Magereza wakisikiliza maelezo ya utambulisho kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim Bw Baddal Calikusu (hayupo pichani)

Mpimaji Ardhi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza,Mrakibu Msaidizi wa Magereza Habibu Yusuph akiwaonesha wajumbe wa Bodi mchoro wa Ramani katika mradi wa ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji cha Gereza Kigongoni kati ya Kampuni ya Tarbim na shirika la Magereza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni mara baada ya Kikao cha kwanza kilichofanyika katika Hoteli ya Green Park iliyopo Mjini Bagamoyo (wa kwanza kulia) ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana(wa tatu kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Masunga

No comments: