Advertisements

Sunday, February 1, 2015

Makamo mwenyekiti wa UTU kuwasili Tanzania

Makamo mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V Mheshimiwa Peter Kazaura kuwasili nchini Tanzania Kesho 02.02.2015 kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kiongozi wa juu wa Taifa. akiwa Tanzania atafanya mazungumzo na uongozi wa mashirika yafuatayo TIC, Basata, Wizara ya Ardhi, NSSF, NHC, Tanzania Diaspora Initiative na Wizara ya Utamaduni Michezo na Vijana.
Mazungumzo hayo yatalenga upatikanaji wa Fursa zilizopo Tanzania kwa Diaspora. akiendelea kueleza msemaji wa Umoja huo Watanzania wanaoishi ujerumani wangependa pia kuhusishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na Afya, Elimu.
naye Mwenyekiti wa Umoja huo Mhe. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha kuwepo kwa safari ya Makamo Mwenyekiti Mhe Peter Kazaura na alisema UTU e.V umechukua uamuzi huo baada ya Watanzania nchini Ujerumani kukosa nafasi ya kuongea na Rais wa Tanzania wakati wa ziara ya Rais nchini Ujerumani.Pia watanzania wanaoishi ujerumani wanaulalamikia ubalozi kuwa viongozi wa umoja wao walinyimwa nafasi ya kuonana na kumsalimia Mhe.Rais Dkt.Jakaya Kikwete.

2 comments:

Anonymous said...

Kwa nini watu wengine wanapenda unnecessary publicities? Au ndiyo "Nshomile mpaka embwa yange ishomile" style?

Anonymous said...

So what?.vijana wenzetu mliopo nje tumieni muda wenu vizuri..kama ni kusoma someni kwa bidii..kama ni kazi fanyen kwa bidii...achaneni na siasa sijui za kumsalimia rais..sijui za kuitana mhe..sijui za kulalamikalalamika....msiwe kama sisi kutwa siasa

Joe
Ilala