ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 27, 2015

Manispaa ya Temeke imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila

Manispaa ya Temeke imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo.

Ama kweli ukistaajabu ya musa hakika utayaona ya firauni...na kuishi kwingi ni kuona mengi..hali kadhalika wahenga wanasema Tembea uyaone...Misemo hiyo mitatu inaweza kujidhihirisha kwa namna tofauti tofauti kupitia tukio la mkazi wa Jiji la Dar es salaam ambaye ni Mwalimu wa kike katika shule ya Sekondari Kibasila iliyopo hatua kadhaa kutoka Manispaa ya Temeke kubainika ndani kwake alipokua akiishi huko Yombo, Kisiwani Kata ya Sandari kuwa kuna shehena ya kinyesi cha binadamu katika ndoo, mabeseni, chupa za soda, maji pamoja na majagi.
Shehena ya kinyesi iliyokuwa chumbani kwa mwalimu huyo.

Pichani juu ni  Wafanyakazi wa usafi wa Manispaa ya Temeke wakibeba kinyesi kwenda kukimwaga baada ya kuvunja nyumba aliyokuwa akiishi Mwalimu Gaudencia Albert.

1 comment:

Anonymous said...

kwa kweli inasikitisha sana,kwa kumuondolea umeme huyu mwalimu. mimi mwenyewe binafsi. Ninamapipa mawili na ninampango wa kuongeza linguine kwa ajili ya kuzalisha umeme. Umeme umekuwa wa tabu sana Dar. nashauri wamruishie umeme wake.