ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 27, 2015

MKE WA DAVID HAINES ATAKA JIHAD JOHN AKAMATWE AKIWA HAI

Mauaji ya kundi la Islamic State

Dragana Haines mke wa David Haines,mamlaka zinapaswa kumsaka na kumkamata akiwa hai mtu aliyemuua mume wake kwa kumchinja baada ya kutekwa na kundi la wapiganaji wa dola ya kiislam Islamic State wakati akifanya kazi na shirika la misaada la Uingereza.Mtu aliyemchinja David Haines na wengine tayari amefahamika kuwa ni Mohamed Emwazi.

Bi.Dragana amesema tangu alipojua kuwa mmewe David amechinjwa alijipa matumaini moyoni mwake kuwa ipo siku muuaji huyo atafahamika na hatimaye kukamatwa.Lakini baada ya kupatika kwa taarifa hizi za muuaji huyo anasema kuwa itakuwa faraja ya pekee kwa familia za kila aliyeuawa kinyama na wauaji hao, kwa sababu kama atakutwa amekufa anaona hicho kitakuwa ni kifo cha heshima kwa Mohamed Emwazi, lakini maombi yake ni kwamba kukamatwa akiwa hai na afe baadaye.


Kwa upande wake Barak Barfi ambaye ni msemaji wa familia ya Sotloff iliyopoteza ndugu yao pia, anasema kuwa hawana wasiwasi juu ya kukamatwa kwake muuaji huyo Mohamed Emwazi ama JIHAD JOHN.

"Tuna Imani kubwa sana na nchi ambayo vyombo vyake vya usalama na kiintelijensia vitawakamata watu hawa.Tungependa kwenda kumuangalia muuaji huyu ana kwa ana wakati wa mashtaka yake katika mahakama ya Marekani,na pia kuona akitumikia kifungo chake, katika gereza maalumu ambako ataishi huko pekee yake katika upweke.hiyo ndiyo sheria ya Marekani na hivyo ndivyo nchi yetu inavyoshughulikia matatizo kama haya"amesema Barak

Mwanaume ambaye amekuwa akitekeleza mauaji ya mateka wa kundi la wapiganaji wa Islamic State ajulikanaye kwa jina la utani "Jihadi John",ametambuliwa.
Bwana huyo ambaye taswira yake akiwachinja mateka kwa kisu bila huruma ndiyo nembo ya wapiganaji hao sasa ametambuliwa kuwa anatokea Uingereza.
Shirika la Habari la BBC limetambua kuwa jina lake kamili ni Mohammed Emwazi.
Emnuazi ameonekana kwenye video kadhaa ya mauwaji ya mateka wa mataifa wa magharibi, akiwemo Mmarekani James Foley, Raia wa Uingereza, Alan Henning na mwaandishi habari wa Japan, Kenji Goto.
Inaaminika kuwa Emwazi ni raia wa Uingereza na hasa anatokea magharibi mwa London.
Yamkini Emnuazi aliyezaliwa Kuwaiti na mwenye umri wa kati ya miaka 20 -29 alikuwa amefahamika sana na vyombo vya usalama lakini kwa sababu za kiusalama haikuwezekana kumtambua.
Anaaminika amewahi kuishi Somalia mnamo mwaka 2006 na anauhusiano mkubwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabab nchini humo.
Polisi nchini Uingereza imeziomba vyombo vya habari kutosambaza habari ambazo hawajazithibitisha kumhusu jamaa huyo kwani uchunguzi unaendelea.
Hata hivyo bado habari za kina kumhusu Jihadi John hazijatolewa.
Mwandishi wa maswala ya Usalama wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa vyombo vya usalama vya serikali za mataifa yanayokaribia Somalia sasa yana kila sababu ya kutahamaki.

Kwa sababu Kuhusika kwake na kundi la Al Shaabab kisha akajiunga na kundi la Islamic State ambalo kwa wakati mmoja lilikuwa linashindana na wanamgambo wa Al Qaeda kuhusu yupi kati yao anayeushawishi
mkubwa
Ishara kuwa Al Shabab inazingatia msimamo mkali wa kidni hata zaidi ya Al Qaeda.
Kwa sababu itakumbukwa kuwa Al Qaeda ilipinga hatua kali ya kuwachinja mateka nchini Iraq na Syria.
Emnuazi ambaye amekuwa akiwabeza mataifa ya Magharibi kabla ya kuwakata shingo naaminika kuwa mtaalamu wa maswala ya kompyuta alisomea chuo kikuu cha Westminster.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC bwana huyo anaaminika kuwa alikwenda Syria mwaka wa 2012, lakini kabla ya wakati huo majasusi wa Uingereza na Marekani walikuwa hawajajua tishio lake.
.-BBC

2 comments:

Anonymous said...

duu hatari

Anonymous said...

Mkuu, haiminiki kwamba jamaa ni raia wa uingereza bali inathibitika ni raia wa uingereza kama jamaa ni yeye ailitajwa, it is no doubt ni British citizen, wenzentu hawabahatishi to prove someones citizenship sio kama nchi zetu za afrika, na pia jamaa hajawahi kuishi somalia bali inahisiswa alikuwa anataka kwenda somalia kujiunga na al shabab na ndio maana alikamatwa dar es salaam airpot na kuzuiwa kuingia Tanzania airport na kurudishwa kwa kuhisiwa ilikuwa ni anatafuta njia ya kwenda somalia