
Bobbi Kristina alipokimbizwa hospitali wakati akiwa na miaka 18 baada ya kuchanganya vilezi muda mchache baada ya kifo cha mama yake kutokea.

Cissy Houston Bibi ya Bobbi Kristina Brown akiwasili hospitali ya Emory siku ya Ijumaa Februari 6, 2015 kumjulia hali mjukuu wake Cissy Houston ni mama mzazi wa Whitney Houston.
Chanzo cha uhakika kutoka familia ya Bobby Brown kimesema msiba wa Whitney Houston tulibaguliwa sana na familia ya Houston na walituletea dharau za dhahili sasa hivi tumeungana, kitu kama hicho kisitokee kwa Bobbi Kristina kama mambo yataenda vinginevyo.
Kwenye msiba wa Whitney Houston Bobby Brown aling'aka baada ya mabaunsa kumzuia kukaa karibu na Bobbi Kristina wakati wa ibada ya mazishi ikiendelea. Wasiwasi wa swala kama lile linaweza kutokea kwani tayari limejitokeza kwenye chumba cha wagonjwa mahututi alicholazwa Bobbi Kristina, familia ya Bobby Brown ni wachache waliopewa nywila (passcode) ya kuingia chumba cha mtoto huyo.
Msemaji mmoja kutoka familia ya Bobby Brown alisikika akisema kama lololte litatokea kwa Bobbi Kristina hawatakubali familia ya Houston watufanye kama watoto na kutubagua huyu mtoto ni wa Bobby Brown na ni kwenye damu yetu.
No comments:
Post a Comment