Watu sita wameuawa kwa moto baada ya nyumba inayomilikiwa na mzee David Mpili, kuteketea kwa moto huko Kipunguni Ukonga jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi Februari 7, 2015. Taarifa zinasema, familia hiyo ambayo ina uhusiano na waziri wa nchi ofisi ya rais kazi maalum, Profesa Mark Mwandosya iliokana na hitilafu ya umeme. profesa Mwandosya mwenyewe ni miongoni mwa wau waliofika kwenye eneo la tukio mapema leo hii Jumamosi, ili kuwapa pole na kujionea uharibifu na maafa yaliyosababishwa na moto huo, pichani majirani ndugu jamaa na marafiki, wakiangua kilio kwenye eneo la ajali mapema leo
Profesa Mark Mwandosya, (Mwenye suti), akiangalia uharibifu uliofanywa na moto huo, alipofika eneo la ajali mapema leo Jumamosi februari 7, 2015
Hii ndiyo hali halisi, mabaki ya nyumba hiyo yakionekana leo jumamosi Februari 7, 2015
Majiranoi wakiondoa mabaki ya nyumba hiyo Picha kwa hisani ya K-VIS




No comments:
Post a Comment