ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 7, 2015

MCHUMBA WA BOBBI KRISTINA HUENDA AKAWA MATATANI


Habari ambazo Vijimambo imezipata, Bobbi Kristina alikutwa na michubuko ambayo bado haijajulikana imetokana na nini japo bado Polisi wanaendelea na uchunguzi ikiwa Nick Gordon na rafiki yake waliokuwepo kwenye tukio wakiwa wamehojiwa na polisi wa jimbo la Georgia.

Polisi inajaribu kutafuta saa moja kabla ya Bobbi Kristina kukutwa bafuni ni nini kilichokua kikiendelea kati ya hao wapenzi wawili. Vijimambo imepata taarifa Max Lomas rafiki ya wawili hao aliyemgundua Bobbi Kristina akiwa ameanguka bafuni, alifika nyumbani kwao majira ya saa 3 asubuhi na kuwa na Nick Gordon kwa muda huo bila ya kumwona Bobbi Kristina huku akiambiwa alikuwa chumbani.

Mida ya saa 4 asubuhi alifika fundi wa kutengeneza waya za TV na alikuwa akihitaji kuingia chumbani kurekebisha tatizo hilo wakati huo Nick Gorgon alikua hajulikani alipo ndipo Max Lomas alipochukua jukumu la kumwingiza fundi huyo chumbani kufanya marekebisho hayo na Max kumkuta Bobbi Kristina akiwa bafuni ameanguka huku kichwa chake kikiwa kimeinamia chini na Max kupiga ukelele wa kuomba msaada ndipo Nick Gordon alipotokea na kujaribu kutoa huduma ya kwanza kwa Bobbi Kristina.

Max Lomas alisema nyumba ya wawili hao ilionekana kama imepigwa deki na kujaribu kusafisha alama za damu iliyokuwepo kwenye sakafu. Habari zingine zinasema Polisi wanataka kumhoji tena Max Lomas kwa mara ya pili ili kuendelea kupata ushahidi wa kutosha kama wawili hao walikwaruzana na kupigana kulikopelekea Bobbi Kristina kuishia kuanguka bafuni na kuzimia.

Nick Gordon na Bobbi Kristina wameishakuwa na ugomvi wa mara kwa mara huko nyuma.

1 comment:

Anonymous said...

na kikulacho kiko muongoni mwakoo. amelelewa vema na vizuri na ka hisani zote na marehemu whitney Houston,na leo hii anataka kumgeukia mwanawe na kuumuuwa kisa pesa. kweli kikulacho kiko miungoni mwakoo.

tahadharini sana nawatu kama hawa wasio na shukran na muwekeni mungu mbele kwa kila jambo lenu.