Advertisements

Monday, February 2, 2015

MTOTO WA WHITNEY HOUSTON, BOBBI KRISTINA ALAZWA HALI YAKE NI TETE

Bobbi Kristina mtoto wa Whitney Houston aliyezaa na Bobby Brown (picha juu) amekutwa ameanguka kifudifudi bafuni na kukimbizwa hospitali siku ya Jumamosi Januari 31.

Bobbi Kristina alikutwa kwenye bafu huku uso wake ukiwa ameinamia chini huku akishindwa kupumua na kukimbizwa hospitali ambapo madaktari wamejaribu kumrudisha katika hali yake ya kawaida ambayo sasa inaonekana ubongo wake unafanyakazi kwa asilimia ya chini kitu ambacho madaktari wamesema sio dalili nzuri kwa mgonjwa wa namna hiyo na kuwaambia familia ya Bobbi Kristina kuendelea kusali na kumwombea Bobbi Kristina apate nafuu haraka.

Baba ya Bobbi Kristina Bobby Brown mwanamuziki aliyetamba enzi hizo akiwa na kundi la New Edition na baadae kujiengua na kuwa peke yake sasa hivi yupo pembeni mwa kitanda cha mwanae akiwa ameacha shughuli zote na kuendelea kumuuguza kwa karibu zaidi mtoto wake.

Whitney Houston kabla ya kifo chake nae alikutwa bafuni akiwa hoi hajiwezi ikiwa amezidiwa na madawa ya kulevya aliyokua amebiya kitu ambacho kilidhaniwa ndicho alichokua amekifanya mtoto wake huyo mara tu alipokuwa amekutwa nae bafuni akiwa amezidiwa huku uso wake ukiwa umeinamia chini huku akishindwa kupumua.

Aliyemgundua ni Nick Gordon ambae ni mchumba wa Bobbi Kristina akiwa na marafiki zake na kutoa taarifa polisi ambao walifika kwenye tukio na baadae waliikagua nyumba ya Bobbi Kristina wakitafuta kama kulikuwa na madawa ya kulevya na kukuta hakuna madawa yaliyopatikana.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema leo Jumatatu madaktari waliendelea na vipimo vya ubongo na madaktari kupata matumaini japo kidogo ubongo umeonyesha dadlili nzuri kidogo jambo ambalo limefufua matuamaini ya madaktari japo wameomba familia na watu wakaribu wazidi kumwombea Bobbi Kristina aendelee kupata nafuu.

No comments: