Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye ofisi za kampuni ya Free Media ltd jijini Dar es salaam, Nape ambaye yupo kwenye ziara ya kutembelea vyombo vya habari nchini leo alitembelea gazeti la Tanzania Daima na Jambo Leo
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye(wa pili kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye ofisi za kampuni ya Free Media ltd jijini Dar es salaam, Nape ambaye yupo kwenye ziara ya kutembelea vyombo vya habari nchini leo alitembelea gazeti la Tanzania Daima na Jambo Leo wengine kwenye picha ni Mkuuwa Mawasiliano ya Umma CCM Makao Makuu Ndugu Daniel Chongolo (kushoto) na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima Ndugu Neville Meena.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na Wahariri na waandishi wa gazeti la Tanzania Daima.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye (kulia) akimuonyesha kalenda ya CCM ya mwaka 2015 Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima Ndugu Neville Meena.
Mhariri wa Tanzania Daima Edson Kamukara akifurahia kalenda ya CCM 2015 waiokabidhiwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye alipowatembelea kwenye ofis za gazeti la Tanzania Daima na kufanya nao mazungumzo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Jambo Leo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JL Communication inayochapisha magazeti ya Jambo leo na StaaSpoti Bw. Theophil Makunga (kushoto) na Kulia ni Meneja Masoko Juma Mabakila.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akimuonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JL Communication inayochapisha magazeti ya Jambo leo na StaaSpoti Bw. Theophil Makunga kalenda ya CCM mwaka 2015 kabla ya kumkabidhi ,Nape yupo kwenye ziara ya vyombo vya habari ikiwa kama sehemu ya utaratibu wake wa kuvitembelea kushauriana, kupeana maoni na kujenga mahusiano.








2 comments:
kanzu na vibaragashea siku hizi mnaviva sana mashallah si haba karibuni kwenye uislamu.dini ya amani.
kwenye dini ya amani??Mmmmhhh! Watata nyie.
Post a Comment