
Foreign Affairs minister Bernard Membe
Ukweli ni kuwa, Mheshimiwa Membe alialikwa na Baraza Kuu la Makanisa ya Sabato Duniani (Seventh Day Adventist - SDA), kufunga tamasha la kanisa hilo lililofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tamasha la siku mbili lilifungiliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Gharib Bilal tarehe 8 Februari, 2015, huku Mheshimiwa Membe akiwa amealikwa kulifunga tarehe 9 February, 2015.
Wakati anatoa salamu zake kwa waumini na wageni wengine walioalikwa kweye hafla hiyo, Mhehimiwa Membe alianza kwa kutambua uwepo wa viongozi wa serikali ambao pia ni waumini wa SDA. Na alianza kwa kumtaja Mheshimiwa Stephen Wassira, aliyekuwepo meza juu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa Masaju, na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Maswi. Mheshimiwa Membe hakusema chochote juu ya viongozi hawa zaidi ya kutambua uwepo wao na kuwatambua wasiokuwepo kama waumini wa SDA. Pia Mheshimiwa Membe hakufanya mahojiano na chombo chochote cha habari kuhusiana na ama tukio lenyewe la SDA au Maswi.
Ni jambo la kusikitisha kuwa gazeti la Mtanzania limeamua ‘kumlisha maneno’ Mheshimiwa Membe, kwa kuandika taarifa ambayo si ya kweli. Na zaidi ya hapo, gazeti hili la Mtanzania limewahoji watu mbalimbali juu ya hiki wanachodai kuwa ni ‘utetezi wa Membe wa mtandao wa ufisadi’ lakini hawakumhoji Waziri Membe mwenyewe ili kupata ukweli wa kile alichosema kwenye shughuli ya waumini wa SDA. Baadhi ya watu waliohojiwa kuhusu taarifa hii potofu ni pamoja na mwenyekiti wa CUF, Prof Lipumba, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mheshimiwa Tundu Lissu (MB), na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson, na wote walionesha kushangazwa kama si kushtushwa na taarifa ambazo kimsingi zinamwonesha Mheshimiwa Membe kuwa anapingana na maazimio ya Bunge!
Mheshimiwa Membe asingependa kuhoji nia au madhumuni ya gazeti la Mtanzania kuandika habari ambazo si za kweli – maana jibu hilo wanalo wenyewe gazeti la Mtanzania. Hata hivyo, Mheshimiwa Membe angependa kuweka kumbukumbu sawa kwa kile alichokisema, kwa kuweka hotuba yake aliyoitoa siku hiyo ya tarehe 9 Februari, 2015 Uwanja wa Taifa. Pia kuna audio kwa wale wanaopenda kusikiliza.
Taarifa hii inatolewa kwa matarajio kwamba uongozi wa gazeti la Mtanzania utachukua hatua stahiki ili kulinda heshma yake mbele ya jamii na pia heshma ya tasnia ya habari nchini.
Before I start my speech, let me also recognize the presence of Honorable Minister Stephen Wassira the Seventh Day Adventist disciple, who has traveled 500 kilometers to be here. Mheshimiwa Wassira karibu sana.
Before I continue with my speech let me also mention other government officials who are also members of the SDA apart from Honorable Wasira;
The Chief Secretary, Hon. Sefue is an SDA member,
The Attorney General of Tanzania Mr. Masaju is an SDA member,
The Permanent Secretary Mr. Maswi of Energy and Mineral, is an SDA member,
So, I mean there are so many others in government that are not only members but they acknowledge many good things that the SDA has been doing.
….continue in English version, see the Swahili translation….
Kwa muhtasari tu kwa Watanzania mlioko wengi, na Watanzania wanaotusikiliza;
Nimemshukuru Rais wa Baraza Kuu la Makanisa ya Sabato Duniani, kwa kujumuika nasi na kuamua Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano hili kubwa sana la bara la Afrika.
Na ni imani yangu kwamba mtapokea salamu hizi nilizotoa kwa niaba ya Serikali…...
Nimemshukuru kwa mwaliko wake kwangu kuja kujumuika nanyi na kufunga Kongamano hili. Nimekubali kwa sababu mbili, kwanza, jambo lenyewe hili la kiroho mnalosimamia na kulifanya ni jambo jema sana kwa ustawi wetu sote. Pili, kongamano hili ni la kimataifa na hivyo linauhusiano na kazi yangu ya uanadiplomasia. Katika miaka 9 ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na miaka 8 ya kuwa Mshauri wa Balozi wa Tanzania nchini Canada, nimejifunza kuwa diplomasia na hofu ya Mungu/imani vikifanya kazi kwa kushirikiana, hakuna changamoto yoyote ya kidunia isiyoweza kukabiliwa. (MAKOFI)
Nimezungumzia uhusiano kati ya Serikali na Dini. Nimesema kuwa vitu hivi viwili havitenganishiki, ni sura mbili za sarafu. Kwa sababu, binadamu ni mwili na roho na kila kimoja hakina budi kuendelezwa. Serikali inashughulika na miili na akili, Dini zinashughulika na roho. Dini na Serikali zikifanya kazi pamoja sawasawa, tutahitaji sheria chache, polisi wachache, magereza machache. Dunia itakuwa mahala pazuri pa kuishi. Tunahitajiana.(MAKOFI)
Wenzetu wa vyombo vya dini wanahubiri amani wanakiri imani, sisi wanadiplomasia na Serikali tunatengeneza amani na wakati mwingine tunatumia vyombo vya dola kuitengeneza hiyo amani. Kwa hiyo lengo letu ni moja, kuleta amani, utulivu, katika nchi. Wenzetu njia yao ni nyembamba --sorry-- ni nyembamba lakini ina mapana na ni nzuri zaidi, kuliko ile tunayoitumia sisi. (MAKOFI)
Lakini diplomasia na dini zinakutana kwenye kukuza amani, ulinzi na usalama duniani.
Lakini pia tunakutana kwenye maadili. Viongozi wanaolelewa vizuri na dini zao, wanakuwa waadilifu. Na SDA ni miongoni mwa dini zinazoweka viongozi wazuri sana wa nchi yetu. (MAKOFI)
Na kwasababu hiyo basi, unapoona diplomasia inatengeneza mahusiano mazuri ya dunia, dunia inaangalia uadilifu kwanza, kama kigezo cha uongozi bora, na kama kigezo cha watu wenye amani na utulivu. Na kawaida Serikali, diplomasia na dini hata Rais mwenyewe, tunakutana tunapozungumzia masuala ya uadilifu wa viongozi wake. (MAKOFI)
Tunzeni hiyo, hubirini uadilifu, na mshiriki katika kutengeneza viongozi bora kwa misingi ya uadilifu. (MAKOFI)
Lakini jingine, nimeshukuru sana Kanisa la Sabato kwa kazi na mwenendo mzuri unaofanywa katika nchi yetu. Unapoona kwamba watu milioni nne waliomo nchini kwetu, wa SDA, wana shule za msingi 10, wana shule za sekondari 15, wana vyuo vikuu 2, wana hospitali kubwa 2, wana vituo vya albino vinavyofanya kazi hapa nchini. (MAKOFI)
Hivi kama kingekua chama cha siasa, nani angeshindwa kuwapa ushindi wa utawala wa nchi hii. (MAKOFI)
Nani angeshindwa kuwapa ushindi. Lakini ukiachia hayo, ni Chama cha Mapinduzi peke yake chenye kumudu kazi hiyo. (MAKOFI, VIGELEGELE, VICHEKO)
Lakini naomba niweke wazi kabisa, kama chombo cha dini, kama SDA, kinajali wananchi wake, kitaacha vipi kupanuka kutoka watu 15,000 mwaka 1960 hadi kufikia watu milioni nne mwaka 2012. (MAKOFI) Wataacha vipi kupanuka na kuwa watu wengi kwa huduma hii, wanayoitoa kwa wananchi. (MAKOFI)
Nawapongeza sana watu wa SDA, mbele ya kiongozi wenu wa dunia, kwa kazi nzuri mnayoifanya na shule mnayofundisha Watanzania kwamba ukitaka kuongoza Watanzania, fanya kama SDA. (MAKOFI)
Nalipongeza kanisa la SDA kuwa mfano mzuri wa ustahimilivu na uvumilivu wa dini na imani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika miaka yangu yote ya nafasi yangu ya uwaziri, na kaka yangu Mzee Wasira ataniunga mkono kwenye hili, sijawahi kusikia mgogoro wa kimatatizo wala mfarakano unaoongozwa na SDA (MAKOFI) dhidi ya madhehebu mengine, au dhidi ya wananchi. (MAKOFI)
Mpo, mnafanya kazi zenu, mnachapa shuguli zenu kwa amani na utulivu, hamjachokoza mtu, na hamtachokoza mtu, na hiyo ni sifa mojawapo ya nchi yenye amani duniani. (MAKOFI)
Hongereni sana wana SDA. (MAKOFI)
Narudia, kama wananchi wote wa dini zote tukiiga mfano wenu, Tanzania tutasonga mbele kama Taifa. (MAKOFI)
Nawashukuruni kwa kunisikiliza na ninawatakia maandalizi mazuri ya kongamano la kidunia litakalofanyika baadae mwaka huu huko Marekani. (MAKOFI)
5 comments:
Nakubaliana na ujumbe wa Mhe Membe vyombo vya habari visitumiwe kujenga tofauiti za kidini.
Mzee Wasira suti yake vipi??????
wasira hilo koti vipi tena...Tanzania...duhhhh
Wassira needs to just RETIRE people.
He looks old, look the way his suit coat/blazer is button?? Whos dressing him up?
Enough is enough.............
Sikubaliani na Waziri Wasira kuvaa koti namna hiyo!
OOOPPPPSSSSS!
Post a Comment