ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 7, 2015

TATIZO LILILOSABABISHA KUFUNGWA KWA KIWANDA CHA CEMENT TANZANIA WAZO HILL

Kiwanda cha Capital Cement San Antonio.TX kilikumbwa na tatizo kama la Wazo hill na T.E.S Kampuni ya Dr Temba Mtanzania mkazi wa New York alipata tenda na alienda kutatua tatizo hilo kwa kufunga filters maalum za kuzuia huo moshi mchafu kusambaa na kusababisha matatizo ya afya kwa wakazi wa eneo la kiwanda. Dr Temba ni engineer anaedesign hizo machine za air pollution system na kampuni yake ya T.E.S uzifunga. Na toka zimefungwa filter hizo tatizo la kutoa moshi mchafu liliisha na sasa kiwanda kina chapa kazi bila tatizo lolote. Nchi yetu inawataalam wengi Diaspora lakini inakuwa vigumu kupata nafasi za kufanya kazi nchini kwetu kutokana na ukiritimba na ubokwenye wa nchi yetu wa kukumbatia na kuthamini wageni kuliko wazawa.
Hiki ndiyo kiwanda cha Wazo Hill kilichofungwa kwa sababu ya moshi mchafu unaosababisha afya ya wakazi wa eneo hilo kuumwa ugonjwa wa TB. Manager wa kiwanda bwana Alfonso kasema wameagiza filter na zinatarajiwa kuwasili mwisho wa mwezi ilikumaliza tatizo hilo la moshi mchafu.
Dr Temba wa T.E.S akiwa Capital Cement San Antonio Texas akifunga machine zake.
Kiwanda cha Capital Cement San Antonio.TX kikifanya kazi baada ya T.E.S kufunga machine zake huwezi kuona moshi wowote ukitoka tena. Wazo hill wanatakiwa kupata machine hizo hili kutatua tatizo la moshi huo.

2 comments:

Anonymous said...

I thin it good idea to shut up instead of keeping complain the same thing everyday. what do you do??? you the so called Diaspora ask yourself.

Anonymous said...

Wee mdau hapo juu bora ungeandika kiswahili tu maana ulichoandika kwa kiingereza hakieleweki