ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 9, 2015

UJUMBE WA KAMPUNI YA SIEMENS KUTOKA AFRIKA YA KUSINI WAMTEMBELEA WAZIRI WA UCHUKUZI

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Siemens, Bi. Sabine Dall’Omo, wakati akifafanua jambo, alipomtembelea Waziri wa Uchukuzi akiwa na ujumbe wake, kutaka kufahamu fursa za uwekezaji katika sehemu ya reli, leo asubuhi.
Wakurugenzi wa Wizara ya uchukuzi, na ujumbe wa kampuni ya Siemens kutoka nchini Afrika Kusini wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Siemens, Bi Sabine Dall’Omo wakati Afisa huyo na Ujumbe wake walipotembelea Wizara ya Uchukuzi, kufahamu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sehemu ya reli leo asubuhi.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Siemens, Bw. Kevin Pillay, akiwasilisha mada, wakati ujumbe wa Kampuni hiyo ulipomtembelea Waziri wa Uchukuzi, leo asubuhi kufahamu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sehemu ya reli.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

No comments: